December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, yaishauri TEMESA kujiendesha kibiashara

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu imefanya ziara mkoani Mwanza na kutembelea miradi ya ukarabati wa Karakana ya Mwanza na vivuko ,inayotekelezwa na serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA).

Huku ikiishauri TEMESA kupitia Mtendaji Mkuu wake,kufanya mabadiliko ya kimfumo ili iweze kujiendesha kibiashara na kutoka huduma zinazowavutia wateja was ndani na nje.

Akizungumza jijini Mwanza mara baada ya Kamati hiyo kukagua Miradi hiyo,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu,Selemani Kakoso amesema ili TEMESA iweze kujiendesha kibiashara na kutoa huduma inayovutia mfumo wake unapaswa kubadilisha.

Amesema kwa vile Mtendaji Mkuu TEMESA ambaye amepewa dhamana na serikali muda mfupi,ndio anaingia kwenye kuisoma TEMESA wanamuomba aubadilishe mfumo ili iweze kubadilika na kutoa huduma ambayo itakuwa kivutio na ijiendeshe kibiashara.

“Ijiendeshe kibiashara maana yake kwanza uwe na mafundi wengi ambao watafanya kazi inayovutia watu na mazingira bora,serikali imekupa fedha ili utengeneze mazingira ambayo yatakuwa kivutio ikiwemo yale maeneo yaliokuwa kama mahabusu,sasa kajipange vizuri Mtendaji Mkuu wa TEMESA,tusikalie tu kuwa mnapata zile fedha ndio mnajiendesha,kabadilisheni mfumo ili ulete uboreshaji ambao utakuwa na manufaa na utakuwa kivutio kwa wateja wa ndani na nje,” amesema Kakoso.

Sanjari na hayo amesema wakandarasi wa ndani(wazawa) wenye uwezo wafanyiwe maboresho kwani wakisimamiwa vizuri wana nafasi ya kuleta uchumi katika nchi huku wakiishauri TEMESA kuhakikisha wanamsimamia kwa ukaribu Mkandarasi Songoro Marine Transport Ltd ili aweze kufanya kazi nzuri zaidi.

Ambapo Mkandarasi huyo anatekeleza mradi wa ukarabati wa kivuko cha Mv.Saba Saba,Mv.Sengerema,Mv.Misungwi pamoja ujenzi wa kivuko kipya Cha kuhudumia Rugezi-Kisorya.

“Nimefurahishwa na Mkandarasi wa kitanzania Songoro, ambapo tukimsimamia tunaweza kutengeneza Watanzania wengi wazuri ambao wanaweza kufanya vitu kubwa,nendeni na mkakati wa kuwafanyia maboresho wakandarasi wa ndani ambao waweze kutengeneza vitu kutoka nje ya nchi,wale tukiwasimamia vizuri wana nafasi ya kuleta uchumi katika nchi yetu,”amesema Kakoso.

Aidha amewataka TEMESA ikajipange upya na kufanyia kazi changamoto na mambo yote waliowaekekeza.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameiambia Kamati hiyo kuwa kivuko cha MV. Sabasaba kinatarajiwa kupelekwa katika eneo la Kigongo – Busisi kama kivuko mbadala ili kivuko cha MV. Misungwi kifanyiwe ukarabati mkubwa na baadae kivuko cha MV. Sabasaba kitapelekwa kuongeza nguvu katika eneo la Nyakaliro – Kome.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TEMESA jijini Mwanza, Mtendaji Mkuu TEMESA Lazaro Kilahala,ameieleza Kamati hiyo kuwa ukarabati wa Karakana ya Mwanza umelenga kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwenye karakana hiyo.

“Mradi huu wa ukarabati wa Karakana ya Mwanza ni kwa ajili ya kuboresha mazingira ya eneo la kutunza vipuru na vilainishi,ofisi ya mafundi wa matengenezo ya umeme wa magari,ofisi ya karakana ya mafundi umeme wa nyumbani na ofisi ya mafundi wa magari huku Mkandarasi wake akiwa Corporation Sole Superintendent wa Mwanza huku gharama ikiwa ni milioni 500.7,”amesema Kilahala.

Aidha kufuatia maelekezo ya kamat hiyo Kilahala,ameahidi kufanyia kazi maelekezo aliyopatiwa pamoja na ofisi yake itaandaa taarifa za kina za utekelezaji wa miradi wanayoisimamia na kuiwasilisha kwenye kikao cha kamati hiyo Bungeni jijini Dodoma.

Kwa upande wake Meneja wa Fedha kutoka Songoro Marine Transport Ltd Mohamed Salum,alielezea Kamati hiyo ilipomtembelea katika Karakana yao kwa ajili ya kugaua na kujionea namna ukarabati wa vivuko unavyoendelea kikiweko cha Mv.Sabasaba amesema,kwa wanaendelea kutekeleza miradi ya TEMESA.

“Miradi inayoendelea kwa hii Yard ya Mwanza kwa sasa tuna huu wa ukarabati wa Mv.Temesa ambao upo kwenye hatua za mwisho, TASAC jana walifanya ukaguzi na kuna mapendekezo walisema tuyafanye na watarudi tena kufanya ukaguzi wa mwisho,ukarabati wa Mv.Musoma ambao vifaa vyake vimeagizwa lakini tuna ukarabati wa Mv.Sabasaba ambao unaendelea vizuri,”amesema Salum.

Vile vile kamati hiyo ipo mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua Miradi mbalimbali mkoani humo ambayo ilipata fursa ya kikagua mradi wa ukarabati wa kivuko cha MV. Sabasaba unaogharimu kiasi cha milioni 239.9,MV. TEMESA kinachotoa huduma kati ya Kirumba na Luchelele jijini Mwanza. Vivuko hivi vyote vinakarabatiwa na kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd ya jijini Mwanza,Karakana ya Mwanza.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso, akizungumza wakati Kamati hiyo ilipomtembelea katika Karakana ya kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya kukagua na kujionea namna utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa vivuko ambavyo unatekelezwa na TEMESA.picha na Judith Ferdinand
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, akizungumza katika kikao cha majumuishi mara baada ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu kumaliza kufanya ziara ya kukagua Miradi mbalimbali mkoani Mwanza inayotekelezwa na TEMESA .picha na Judith Ferdinand
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Lazaro Kilahala,akiwasili taarifa ya utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa vivuko na Karakana inayotekelezwa na TEMESA mkoani Mwanza mbele ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ilipomtembelea miradi hiyo mkoani Mwanza.picha na Judith Ferdinand
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti wake Seleman Kasoso,wakiwa ndani ya kivuko cha Mv.TEMESA ambacho ni miongoni mwa vivuko vinavyofanyiwa ukarabati na Mkandarasi Songoro Marine Transport Ltd wakati walipotembelea eneo hilo ili kujionea utekelezaji unavyoendelea. picha na Judith Ferdinand
Meneja wa Fedha kutoka Songoro Marine Transport Ltd Mohamed Salum, akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipomtembelea ofisini kwao kwa ajili ya kujionea namna utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa vivuko unaotekelezwa na serikali kupitia TEMESA unavyoendelea.picha na Judith Ferdinand