November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yapitisha makadirio ya bajeti ya fedha ya mwaka 2022/2023 ya Ofisi ya Waziri Mkuu , Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kujadili na kupitisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 na makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 katika ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
Sehemu ya wakuu wa taasisi pamoja na wakuu wa idara wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia wasilisho la kikao cha kujadili na kupitisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 na makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
Kaimu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Emmanuel Mwakasaka (Mb) akichangia hoja katika kikao hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akijibu hoja wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kujadili na kupitisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 na makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria cha Taasisi ya wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (Osha) Nd. Netiwe Mhando akitoa Mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa lengo la kuwajengea uelewa wa taasisi hiyo.
Meneja wa Mipango na Utafiti wa Taasisi ya Mfuko wa Fidia kwa Mfanyakazi (WCF) Patrick Ngwila akitoa Mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa lengo la kuwajengea uelewa wa taasisi hiyo.