Na Mwandishi wetu,TimesMajira Online, Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Uratibu wa Operesheni Anwani za Makazi ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu  ameongoza kikao cha tisa cha kamati hiyo.
Kikao hicho kimefanyika Juni 02, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali , Wakurugenzi wa Taasisi na wataalamu ambapo wamejadili hatua zilizofikiwa kuhakikisha zoezi la uwekaji wa anwani katika makazi linakamilika kama lilivyokusudiwa.
Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia TAMISEMI,Ramadhan Kailima, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kaspar Mmmuya, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF),Justina Mashiba na Mratibu Anwani za Makazi Zanzibar, Abdalla Dai Abdalla.
Aidha Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika 23 Agosti 2022 nchini ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato