March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kalamu imeongea, Mama Samia siyo wa kelele, bali ni wa matokeo

*Ametufungulia dunia, sasa anatupeleka mbele kwa kasi mpya

Na Costantine Magavilla,Timesmajiraonline

TANGU mwaka wake wa kwanza madarakani, Rais Samia alipa kipaumbele diplomasia ya kiuchumi kama chombo cha maendeleo—si siasa tu.

Royal Tour haikuwa tu onesho, ilikuwani mkakati wa kiuchumi athari zake chanya ni kubwa.

Idadi ya watalii wa kimataifa iliongezeka kwa asilimia132 ikifikia zaidi ya milioni 2.1 mwaka 2024. Mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka dola milioni 700 hadi dola bilioni 3.9
(takriban sh. trilioni 10.14).

Zaidi ya kampuni 850 mpya za utalii na waongozaji watalii zilisajiliwa na kupewa leseni, waongooza watalii 2,800 waliongezeka—ikiimarisha taswira ya Tanzania kimataifa na sekta ya huduma.

Hii siyo diplomasia ya kelele—ni diplomasia ya matokeo. Kama alivyo ahidi Mama Samia ametufungua nchi.

Miundombinu Jumuishi kwa Maendeleo Jumuishi
Pamoja kuendeleza ujenzi wa miundombinu kwa kasi mtazamo wa Rais Samia kwa miundombinu unaweka mwananchi mbele.

Serikali yake imeendeleza miradi inayoambatanisha uwekezaji kwenye vitu unauwishwa na maendeleo ya watu:

Daraja la Kigongo–Busisi, limekamilika kwa asilimia 100 tayari amezinduliwa Juni 19, mwaka huu, uwekezaji wa ndani wa dola milioni 300 unaotarajiwa kuongeza dola bilioni 1.2 kwenye
Pato la Taifa.

Minara mipya ya mawasiliano 8,500 imefungwa, ikifungua fursa kwa maeneo ya mbali. Vijiji 3,731 vimeunganishwa na umeme ndani ya miaka minne ongezeko la asilimia 44.

Huu ni uwekezaji wa kimkakati unaolenga kuunganisha wananchi wote bila kelele, bali kwa vitendo.

Kuwawezesha wanyonge sio tu wenye uwezo mkubwa Ajenda ya kiuchumi ya Mama Samia inalenga walio wengi, Wachimbaji wadogo sasa huchangia asilimia 40 ya mapato ya madini—sh. bilioni 464 mwaka 2024/25 zaidi ya mara mbili wakati anaingia.

Usafirishaji wa nyama nje umeongezeka hadi tani 14,701, ukileta mapato ya dola milioni 61 ukitokea kwenye 1.744 wakati anaingia.

Sekta ya uvuvi sasa inawawezesha Watanzania milioni 6 kupitia uwekezaji katika vizimba, boti na maghala ya baridi; yote haya ndani ya miaka minne ya utawala wake.

Mama anabadilisha maisha ya watu wa kawaida si kwa maneno, bali kwa sera madhubuti.

***Elimu na Vijana: Dira ya Muda Mrefu

Rais Samia amewekeza kwa kiwango kikubwa katika rasilimali watu,
elimu bure hadi kidato cha sita kutoka sh. bilioni 312 hadi sh. bilioni 796.

Madarasa 60,000 mapya yamejengwa, Wasanii 1,370 wamepata fursa ya kimataifa ongezeko mara kumi kutokana maguezi
makubwa BASATA ambayo chini ya Mama Samia imebadilika na kuwa kimbilio la wasanii wote.

Kwa Mama Samia, elimu na vipaji si mapambo ya siasa ni msingi wa ushindani wa kitaifa.

***Utulivu Uliojaa Dira

Licha ya mfumuko wa bei duniani, janga la COVID-19, na athari za tabianchi, Rais Samia ameongoza kwa weledi: Uchumi umedhibitiwa, deni la taifa limewekwa kwenye mizani, uwekezaji wa kijamii umeendelea

Kupitia Dira ya Taifa ya 2050, Serikali yake inajielekeza katik viwanda rafiki kwa mazingira, ajira kwa vijana, kilimo cha kisasa, thamani ya ndani ya bidhaa.

“Hii si siasa ya muda mfupi ni uongozi wa kuona mbali.”

***Hitimisho

Uongozi wa Matokeo, Siyo Maneno

Mtindo wa uongozi wa Mama Samia tulivu, shirikishi na makini—hauitaji makelele ya majukwaani. Uhalisia wake umejidhihirisha kwa
kuifungua Tanzania kwa dunia kurejesha huduma kwa watu kuweka kipaumbele usawa, ubunifu na uendelevu

Kwa wanaouliza alama kuu ya Mama Samia, jibu ni matokeo bila kelele, mifumo bila vurugu. Kalamu imeongea: Mama Samia siyo wa kelele – ni wa matokeo. Ametufungulia