Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Anjela Kairuki amewaagiza viongozi wa Tume ya Utumishi wa Walimu Nchini (TSC) walimu wote wanapata stahiki zao ikiwemo kupandishwa madaraja kwa wakati bila kuwadai pesa.
Waziri Kairuki ametoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Watumishi wa TSC kutoka wilaya zote na Maafisa Utumishi kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara huku akisema wenye tabia ya kudai pesa ndipo washughulikie changamoto za walimu wanaharibu sifa ya utumishi wa umma.
“Sisi tupo kwa niaba ya walimu wenzetu,hebu kila mmoja hapo avae viatu vya wengine,kwa hiyo wakati tunalihudumia kundi la walimu tusiangalie wala kudai chochote,ila tuangalie kile ambacho mwalimu husika anakistahili.”amesema Kairuki
Ameongeza kuwa”Timizeni wajibu wenu kuwasaidia wenzenu siyo lazima wawape pesa ,wenye tabia hiyo mnaharibu sifa ya utumishi wa umma ,nataka walimu wote wapate stahiki zao.
Ameagiza taarifa za walimu wanaostahili kupandishwa cheo na hakuwapanda kwa sababu mbalimbali,ziwasilishwe kwenye mamlaka husika kwa ajili ya hatua zaidi huku akiagiza madai ya walimu yaingizwe kwenye mfumo wa kiutumishi na yasilishwe TAMISEMI.
“Lakini pia fuatilieni madai ya uhamisho na likizo ili walimu walipwe madai yao kwa wakati ,ili wafanye kazi kwa utulivu.”amesisitiza Kairuki
Katika hatua nyingine amewataka washiriki hao wa mafunzo hayo kuagalia dosari zote zinazolalamikiwa na walimu na kuzirekebisha ili wakati wa upandishaji vyeo walimu wote wapande kulingana na wanavyostahili.
“Pia oneni umuhimu wa kuwatembelea walimu katika vituo vyao vya kazi ili kujua changamoto zao badala ya kusubiri mpaka wawafuate maofisini
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato