May 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kadinali Robert Prevost achaguliwa kuwa Papa Leo wa XIV

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Kardinali Robert Prevost amechaguliwa kuwa Papa mpya Leo XIV, akiweka historia ya kuwa papa wa kwanza mzaliwa wa Marekani.
Kadinali huyo mwenye umri wa miaka 69, mwenye asili ya Chicago, Marekani, anasemekana kuwa alitumia muda mwingi wa kazi yake ya ukasisi nchini Peru, ambako aliwahi kuwa Askofu wa Chiclayo.


Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Vatican, baada ya Baba Mtakatifu Francisko kuaga dunia tarehe 21 Aprili 2025.
Moshi mweupe ulionekana ukipanda kutoka katika Kanisa la Sistine Chapel, kuashiria kwamba Makardinali wamefikia uamuzi.
Zaidi ya watu 50,000 walikusanyika katika uwanja wa St. Peter kushuhudia tukio hilo la kihistoria.


Prevost anajulikana kwa mtazamo wake wa wastani ndani ya Kanisa Katoliki, kusawazisha kati ya vikundi vinavyoendelea na vya kihafidhina.