Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
KADA wa Chama cha Mapinduzi CCM Selemani Kaniki ,ameunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwekeza sekta ya Elimu Zingiziwa.
Kada Selemani Kaniki alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Ibanzi Day Care &Primary Academy iliyopo Zogoali kata ya Zingiziwa wilayani Ilala.
Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kada Selemani Kaniki alichangia ujenzi wa shule hiyo mifuko 20 ya sementi na Mbunge wa jimbo la Ukonga Jery Silaa, alichangia mifuko 30 kwa ajili ya shule hiyo ambapo mwaka 2024 inatarajia kuanza darasa la kwanza.
“Naunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya elimu nachangia mifuko 20 ya sementi kuendeleza ujenzi wa shule ili jamii ya Zogoali waweze kusoma karibu na makazi yao “alisema Kaniki.
Kada Kaniki pia aliomba kuwa Mlezi wa shule hiyo ili kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali ambapo pia katika sekta ya michezo aliwachangia jezi seti moja na mipira kumi kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo waweze kushiriki michezo .
Wengine waliojitoa kuchangia shule hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde ,alitatua changamoto live kwa kupigiwa simu ya Kiganjani ambapo Mwenyekiti Side alisema ataleta Bendera ya Taifa, Picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na picha ya Rais Mstaafu Juliaus Nyerere, ambapo Mwenyekiti Side alisema atazikabidhi hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Ukonga Jery Silaa alituma salam zake akisema yupo tayari kumsaidia Mkurugenzi wa shule hiyo changamoto moto zozote za Ardhi ikiwemo kumsaidia kupata hati miliki ya eneo la shule hiyo.
Aidha pia alisema wanafunzi wa shule hiyo wakiumia au kupata majeraha watakuwa wanapewa huduma ya zarula Pridayo Medical Clinic muda wowote watapokelewa wajitambulishe wametoka shule hiyo.
Aliwataka Wazazi wa Watoto wanaosoma shule hiyo kumuunga mkono Mkurugenzi wa shule hiyo kwa kulipa ada kwa wakati ili malengo yao yaweze kutimia na kufikia malengo huku wakijenga ukaribu na walimu katika kufatilia maendeleo ya wanafunzi wao shuleni.
“Nawaomba Wazazi mshirikiane na walimu ,pia muonyeshe upendo kwa watoto kila wakati kwani watoto wadogo wanafamu kila kitu hivyo wanatakiwa kulelewa katika misingi imara wasiingie katika mmomonyoko wa maadili “alisema.
Mkurugenzi wa shule ya kisasa ya Ibanzi Day Care &Primary Academy Rose Sanga alisema shule hiyo ina wanafunzi 87 kati yao wanafunzi 21 wanahitimu elimu ya awali tayari kwa kujiunga elimu ya msingi January 2024.
Mkurugenzi Rose Sanga alisema wanajivunia mafanikio kitaaluma watoto wao wamewapatia maarifa ya ujuzi na stadi mbali mbali ambazo zitawezesha kuendelea hatua nyingine za kielimu
Alisema watoto wa kituo hicho cha Ibanzi Day Care wakilelewa katika malezi mema na maadili mazuri ili kujenga kizazi bora
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi