January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kada Kaniki kujenga kituo cha kisasa cha Polisi Zingiziwa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Kada wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya Ilala Selemani Kaniki amesema mikakati yake katika kata ya Zingiziwa kujenga kituo cha kisasa cha Polisi daraja C ambacho kitakuwa kinatumika na wananchi wa eneo hilo.

Kada Selemani Kaniki , alisema hayo katika mkutano maalum aliyoandaa wakati akizungumza na wananchi wa Zingiziwa alipokuwa akigawa radio za Mawasiliano za kisasa kwa ajili ya Ulinzi shirikishi.

“Nimeguswa katika kusaidia Serikali ya awamu ya sita kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan , kuleta maendeleo kwa wananchi kuwasogezea huduma za kijamii kwa ajili ya kuakikisha usalama unapatikana wakati wote naomba Diwani wa Zingiziwa Maige Maganga unitafutie eneo kwa ajili ya kujenga kituo cha Polisi ambacho kitakuwa kinatoa huduma zote “alisema Kaniki .

Alisema kata ya Zingiziwa ndio kata ya kwanza yenye kwa Walinzi shirikishi watatumia Radio za kisasa za Mawasiliano wawapo katika ulinzi ambapo alikabidhi Radio za Mawasiliano, Tochi,Sare za ulinzi .

Selemani Kaniki alisema amekuwa msaada mkubwa katika kuisaidia Serikali katika mambo mbali mbali ikiwemo kuinua sekta ya michezo wilaya yote ya Ilala kwa kusaidia vijana waweze kushiriki michezo na kujenga afya na umoja kwani michezo ni ajira.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala ASP, Yustino John Mgonja, alimpongeza Selemani Kaniki kwa kusaidia Serikali ususani Jeshi la Polisi katika kusaidia huduma mbali mbali karibu na Jamii.

Kamanda wa Mkoa wa Ilala ASP Mgonja, alisema jeshi lake la Polisi Ilala linaunga mkono juhudi zake litatoa Ramani ya ujenzi wa kituo cha Polisi na kutoa baraka zote za ujenzi huo.

Kamanda ASP Mgonja alisema kazi anazofanya Selemani Kaniki ndani ya kata ya Zingiziwa atafikisha Salaam kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Ilala ambayo inaongozwa na Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo pamoja na Mkuu wa Jeshi Polisi nchini IGP na Kamanda wa Kanda Maalum Jumanne.

Alisema haya aliyofanya Selemani Kaniki ni makubwa amewataka wananchi na wadau wengine kumuunga mkono

Katika hatua Kamanda Mgonja aliwataka wananchi wa Wilaya ya Ilala wasifumbie vitendo vya unyanyasaji na ukatili endapo kutatokea taarifa za ukatili wa Kijinsia watoe taarifa katika vituo vya Polisi, Wilaya ya Polisi Chanika Zingiziwa, Polisi Tabata ,Stakishari na Ilala vituo vyote hivyo vina madawati ya Kijinsia .

Diwani wa Kata ya Zingiziwa wilayani Ilala Maige Maganga alimpongeza Selemani Kaniki kwa kushirikiana na Serikali Pamoja ambapo alisema yupo tayari kupokea wadau wengine wa maendeleo katika hiyo kwani peke yake awezi hivyo wote watakaokuja atashirikiana nao.

Diwani Maige Maganga alisema eneo limeshapatikana kwa ajili ya kujenga kituo cha Polisi hivyo atampa ushirikiano Kada Selemani Kaniki kufanikisha ujenzi huo.

Aidha Diwani Maige Maganga alisema kwa sasa Zingiziwa ipo salama katika maswala ya ulinzi na usalama kazi nzuri inafanywa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika ikiongozwa na Kamanda OCD wa Chanika SP Awadhi Chiko .