November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

KACU chaendelea kufanya maendeleo katika sekta ya kilimo

Na David John, TimesMajira Online

CHAMA cha ushirika KACU wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga kimesema kuwa chama hicho ni moja ya vyama vinavyofanya vizuri sana katika tasnia ya kilimo na kimekuwa chama cha mfano na cha kuigwa katika ushirika.

Amesema chama chao kina vyama vya msingi AMCOS 126 na AMCOS hizo zinajihusisha na mazao ya aina mbili ambapo Kuna zao la biashara ambalo ni tumbaku na zao la Pamba na vyama 46 vinajishughulisha na zao la tumbaku na vinavyobaki vinajishughulisha na zao la Pamba na mazao mchanganyiko.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake mwanzoni mwa wiki hii Mwenyekiti wa Chama hicho cha Ushirika Hamis Majogoro amesema kuwa katika msimu huu wa kilimo wa 2021/22 na 2022 /23 wameweza kuhudumia wakulima katika zao la Pamba ambapo chama hicho kinahusika pia na ununuzi wa zao hilo la Pamba.

Amefafanua kuwa katika msimu huo wa 2021 /22 bei ya Serikali ilikuwa 1500 lakini kulingana na chama kikuu cha Ushirika KACU na vyama vingine ikiwemo chama cha MBCU na chama kikuu cha Ushirika mkoani Geita viliiweza kusukuma bei hiyo kutoka 1500 hadi 2020 kwahiyo wakulima Kwa msimu huu wameweza kufanya vizuri na wakiunga juhudi zinazofanywa na na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Akizungumzia zao la tumbaku Mwenyekiti huyo amesema tumbaku kupitia vyama 46 vinavyolima vimefanya vizuri sana katika msimu huu na Kwa bahati nzuri Serikali iliweza kufungua mianya ya Kampuni kuingia na kuleta Chachu kubwa ambayo imewasaidia wakulima kunufaika na zao hilo la tumbaku.

” Katika kipindi cha nyuma bei ilikuwa ndogo sana lakini baada ya kuingia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye anajali sekta ya kilimo amefanikisha kuingia makampuni makubwa na Kampuni ya Mkwawa life na Kampuni ya wholesafe ambapo kampuni ya Mkwawa life imeweza kuleta Chachu kubwa iliyowasaidia sana wakulima mpaka kufikia kuuza katika wastani wa Dola 2 kutoka Dola.”amesema Majogoro.

Ameongeza kuwa wanaipongeza Serikali Kwa kuweza kufanya kazi kubwa na kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kwani Kwa upande wakulima ambayo sio wa mazao ya biashara pembejeo za ruzuku zinapatikana Kwa urahisi mfano katika wilaya ya kahama Kuna mawakala wengi wanaohudumia na wakulima wanapata oembejeo za ruzuku.

Amesema kuwa Serikali inafanya kazi vizuri na inawajali sana wakulima nchini lakini pia wanajuhudi kubwa ya kuweza kuinua kilimo cha Pamba nchini na Serikali imeweza kuwezesha chama kikuu cha Ushirika KACU kuweza kupewa fedha kununua oil mill Kwa maana ya kiwanda cha kusindika mafuta ya Kula na lengo lake nikuhitaji kuona zao la Pamba linapata thamani na kwamba pindi Soko la dunia linaposhuka wawe na uwezo wa kununua Pamba kutoka Kwa wakulima .

Pia akizungumzia ukamilifu wa kiwanda hicho mashudu yatakayokuwa yanapatikana watakamua sabuni na makapi watatengeneza mkaa kwahiyo Kwa kupitia benki ya maendeleo TAB wameweza kupata mkopo wa shilingi bilioni 3.4 na kwakuazia mwezi februali wataaza ujenzi hivyo wanaishukuri Serikali Kwa hayo wanayofanya katika sekta ya kilimo.

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika KACU Wilaya ya kahama,mkoa wa Shinyanga Hamis Majogoro akizungumza mbele ya waandishi wa Habari hawapo picha kuhusu majukumu na utendaji wa Chama hicho cha Ushirika Kwa wanachama wake (wakulima)