Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Meneja wa Kampeni za Mgombea Urais wa ACT Wazalendo, Ismail Jussa Ladhu, akionesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho, akisema ndicho kinachobeba dira ya mabadiliko ya kweli kwa Zanzibar.
Amesema Ilani hiyo imejaa majibu ya changamoto zinazowakabili Wazanzibari, ikiwemo suala la ajira kwa vijana, huduma bora za afya, elimu yenye ubora na usawa, pamoja na kukuza uchumi wa visiwa kwa misingi ya haki na ushirikishwaji.
Jussa ameeleza kuwa ACT Wazalendo haitabiri mabadiliko, bali imeyapanga kwa vitendo, kupitia mipango thabiti iliyomo katika Ilani hiyo.

Amesema Jussa kwa hamasa kubwa mbele ya umati wa wananchi kuwa Ilani hiyo ndiyo dira ya Zanzibar mpya yenye matumaini, uchumi wa watu na Serikali inayowajali wananchi wake.
Ilani hiyo inatumika kama mwongozo wa hatua zitakazochukuliwa na Serikali ya ACT Wazalendo mara baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, ikilenga kujenga taifa lenye haki, usawa na maendeleo endelevu kwa wote.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako