Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala imepongezwa kwa kuanzisha mashindano ya Jumuiya kila kata kwa ajili ya kujenga chama na Jumuiya ya Wazazi.
Akizungumza katika madhindano ya Jumuiya ya Wazazi kata ya Ilala Leo Katibu wa chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Franta Katumwa, alisema Michezo ni ajira pia Michezo ni Afya pia ujenga mahusiano amezitaka timu zinazoshiriki mashibdano ya wazazi kata ya Ilala kucheza mpira ili iweze kufanya vizuri katika mashindano yao.
“Napongeza Jumuiya ya Wazazi kata ya Ilala Wilaya ya Ilala kwa mashindano haya mazuri ,pamoja na Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala kwa kushirikiana na chama cha Mapinduzi Kata ya Ilala Naona viongozi wote wa Kata wa CCM wanafatilia mashindano haya ” alisema Katumwa .
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala amewataka Jumuiya ya Wazazi washikamane wachape kazi katika kujenga umoja
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM kata ya Ilala Sabry Abdalah , alisema mashindano hayo yameshirikisha timu kumi kila timu inatoa timu mbili kuingia Nusu Fainali mashindano yatamalizika Mei 13 mwaka huu.
Mwenyekiti Sabry Abdalah alitaja zawadi katika mashindano ngazi ya kata alisema mshindi wa kwanza Pesa sh,400,000/=jezi seti Moja na mipira miwili .
Aidha alisema mshindi wa pili atapewa sh,300,000/= na mipira,miwili na mshindi wa tatu shilingi 100,000/=mipira miwili.
Mwenyekiti Sabry amewataka vijana wa Kata ya Ilala kudumisha nidhamu Katika Michezo yao kwa ajili ya kujenga Siasa safi na mahusiano ndani ya Jamii .
Alisema mashindano hayo yameshirikisha timu 10 kwa ajili ya kutafuta wachezaji Bora wa timu ya Jimbo la Ilala waweze kushiriki mashindano ya Jimbo Jumuiya ya wazazi mkoa Dar es Salaam .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba