December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jumuiya ya Wazazi kata ya Ilala wakabidhi wheel chair kwa watu wenye mahitaji Maalum

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Jumuiya ya Wazazi kata ya Ilala imetoa baskeli ya miguu miwili weel chair kwa watu wenye mahitaji Maalum kwa kushirikiana na Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi Imran Jaffar katika mitaa miwili .

Msaada huo ulitolewa jana na Jumuiya ya wazazi na kamati yake ya Utekelezaji kata ya Ilala ambapo walitoa weel chair katika mitaa miwili Mtaa wa Shauri moyo na Mtaa Bungoni .

“Jumuiya yetu ya wazazi iliwafikia walengwa wote wa mahitaji maalum na kuona changamoto zao tuliambatana na Katibu wa CCM kata Devotha Bantulaki na Diwani wa Viti Maalum Aisha Issa alisema Sabry .

Mwenyekiti Sabry alisema mara baada ya kutoa misaada hiyo walifanya ziara Shule ya Sekondari Msimbazi kuangalia athari za mvua iliyonyesha Dar es Salaam juzi.

Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala Imran Jaffar alisema anashirikiana na Jumuiya ya Wazazi katika kujenga chama na Jumuiya ikiwemo pamoja na kuisaidia Jamii .