December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jumuiya ya Wazazi Ilala yakabidhi vifaa vya shule

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala imekabidhi daftari za shule box tatu shule ya Msingi Buguruni Moto Kwa ajili ya kukuza sekta ya elimu .

Msaada huo ulikabidhiwa shule hapo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wa
Kata ya Ilala Sabry Abdalah ,baada kupokea mwaliko kutoka kwa Diwani wa Buguruni Busoro Pazi .

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Wazazi Sabry Abdalah, alisema Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala inaunga mkono Juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuunga mkono sekta ya elimu sera wa elimu bila malipo.

“Ziara hii ya Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala shule ya Msingi Buguruni Moto tunashirikiana na Mlezi wa Jumuiya ya wazazi Imran Jaffar ,Jumuiya yetu Ina jukumu la kusimamia elimu ,Malezi na Mazingira ” alisema Sabry .

Mwenyekiti Sabry alisema wameonyesha ushirikiano kwa Diwani wa Buguruni Busoro Pazi katika Maswala ya elimu ugawaji wa box tatu za madaftari Wanafunzi waweze kusoma kwa bidii kukuza taaluma.

Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi Ilala IMRAN JAFFAR alisema wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani Pamoja na kusimamia sekta ya elimu nchini.