November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jumuiya ya watumiaji maji watahadharishwa Singida

Na Nathanael Limu,TimesMajira online,Iramba

SERIKALI mkoani Singida imezitahadharisha Jumuiya za watumiaji maji kutumia vizuri fedha za makusanyo yanayotokana na kuuza maji na kwa malengo yaliyokusudiwa, kinyume na hivyo, watakuwa halali kwa TAKUKURU.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida,Emmanuel Luhahula akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya maji duniani uliofanyika kimkoa katika kijiji cha Songambele juzi.

Tahadhari hiyo imetolewa juzi na Emmanuel Lutahula Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati akizungumza kwenye hafla ya kuzindua mradi wa maji Kata ya Songambele Jimbo la Iramba Mgharibi. Uzinduzi huu ni maadhimisho ya wiki ya maji duniani.

Amesema jumuiya hizo zinapewa jukumu la kukusanya fedha zinazotokana na jukumu la kukusanya fedha zinazotokana na mauzo ya maji, lengo lake ni huduma ya maji iwe endelevu.”

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida,Emmanuel Luhahula akizindua tanki la kuhifadhia maji katika kijiji cha Songambele juzi ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya maji duniani.

Makusanyo hayo ya fedha,ni kwa ajili ya kugharamia matengenezo ya mashine ya kusukuma maji.Pia mafuta na mambo mengine muhimu ya mradi wa maji kwa ujumla fedha hizo zitumike kwa mambo yaliyokusudiwa.Zikitumika kwa mambo ambayo hayajakusudiwa mhusika/wahusika watachukua hatua kali za kisheri.

Aidha,Luhahula ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, wakati akizindua mradi wa maji wa kijiji cha Ulemo na Misigiri, aliagiza miradi ya maji itunzwe na kulindwa kama mboni ya jicho.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida,Lucy Boniface Shee akimtwisha ndoo ya maji mama mkazi wa kijiji cha Songambele wilaya ya Iramba juzi ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya maji duniani.Wa pili kushoto (suti ya bluu) Mkurugenzi mtendaji wa SUWASA,Singida, mhandisi Patrick Nzamba akishuhudia tukio hilo.Picha na Nathaniel Limu.

Amesema kuwa miradi hii ya maji inagharimu fedha nyingi za Umma. Ni lazima itunzwe ili maji nayo yawatunze wananchi. Naomba nitumie nafasi hii kuiomba SUWASA ikarabati tanki dogo ili maji yake yaweze kutumika kwa Shule ya Sekondari na Msingi.

Kaimu Mkuu wa Mkoa huyo, ametumia fursa hiyo, kumshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake ya kuboresha huduma ya maji aliyoitoa katika kijiji cha Misigiri wakati wa Kampuni.

Katibu CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniface Shee,amesema miradi ya maji ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kifungu cha 147 hadi 149.

“Maji ni uhai bila maji hakuna uhai kwa viumbe vyote hai akiwemo binadamu.Binadamu ana matumizi mengi ambayo ni pamoja na kutumika kuosha mwili wa binadamu kabla hajazikwa, kwa hiyo CCM inasisitiza miradi ya maji itunzwe kikamilifu,’amesema Lucy.

Awali Mkurugenzi mtendaji mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Singida,Injinia Patrick Nzamba,amesema mradi wa maji wa kijiji cha Misigiri na Ulemo unakisima ambacho kiligharimu zaidi ya shilingi 569.2 milioni hadi sasa zaidi ya shilingi 240.9 zimekwisha kupokelewa.

Amesema mradi huo wa awamu ya pili unatekelezwa kwa njia ya manunuzi (force account),umeanza kutekelezwa February nane mwaka huu, na unatarajiwa kukamilika juni nane.

Injinia Nzamba amesema mradi huo ukikamika,unategemea kutoa huduma ya maji safi na salama, kwa wa kazi 9, 960 wa vijiji vya Ulemo na Misigiri.

“Serikali kupitia Wizara ya Maji ina nia ya dhati kuhakikisha wananchi wa vijiji vya Ulemo na Misigiri,wanapata huduma ya maji safi na salama. Tunatoa wito kwa wadau wote wa sekta ya maji tushirikiane kuhakikisha tunafanikisha utekelezaji wa mradi huu,” amesema.

Kauli mbiu ya wiki ya maji mwaka huu, ni ‘Thamani ya maji kwa uhai na maendeleo’