December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Juliano Balletti alivyomaliza ziara yake Dar

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil aliyewahi kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2002, Juliano Balletti, akiinua kombe na kupunga mkono kuwaaga watanzania ikiwa ni ishara ya kushukuru baada ya kumaliza salama ziara yake ya siku mbili na Kombe hilo nchini, wakati akiondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Meneja Masoko wa Cocacola Tanzania, Kabula Nshimbo (kushoto) akimwelekeza jambo mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil aliyewahi kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2002, Juliano Balletti, wakati walipokuwa katika Viwanja vya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam, jana mchezaji huyo pamoja na ujumbe ulioongozana na Kombe la Dunia walipokuwa wakiondoka nchini baada ya kumaliza ziara yao ya siku mbili nchini.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil aliyewahi kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2002, Juliano Balletti (katikati) akicheza ngoma pamoja na wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Elimisha chenye maskani yake Kiwalani jijini Dar es Salaam, wakati mchezaji huyo alipowasili katika Viwanja vya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere akiondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya siku mbili ya Kombe la Dunia.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil aliyewahi kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2002, Juliano Balletti (katikati) akipiga Ngoma pamoja na wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Elimisha chenye maskani yake Kiwalani jijini Dar es Salaam, wakati mchezaji huyo alipowasili katika Viwanja vya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere akiondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya siku mbili ya Kombe la Dunia.
Meneja Masoko wa Cocacola Tanzania, Kabula Nshimbo (wa pili kulia) na mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil aliyewahi kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2002, Juliano Balletti (kulia) pamoja na baadhi ya viongozi wakifurahia jambo wakati wakiangalia burudani ya ngoma kutoka kwa kikundi cha Sanaa cha Elimisha walipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juoius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam, jana mchezaji huyo alipokuwa akiondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya siku mbili ya Kombe la Dunia.
Meneja Masoko wa Cocacola Tanzania, Kabula Nshimbo (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Cocacola na viongozi walioongozana na Kombe la Dunia wakati wakiwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakiondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya siku mbili ya Kombe hilo nchini.
Ndege iliyobeba msafara wa ujio wa Kombe la Dunia ikimwagiwa maji na magari ya Zimamoto ikiwa ni ishara ya Heshima baada ya Kombe hilo kutua nchini na kumaliza ziara yake ya simu mbili.