Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar
JUKWAA la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Ilala wameazimia kumuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Watanzania ambaye ni Mlezi wa Jukwaa Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan ,katika uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani.
Akizungumza katika Kongamano la Wanawake wa Jukwaa Halmashauri ya jiji la Dar Rehema Sanga,amesema maazimio ya Wanawake wa Wilaya ya Ilala ni kusimama na Dkt. Samia kwani amesimama imara katika kuliongoza Taifa.
Sanga amesema Wanawake wilaya ya Ilala wanaunga mkono juhudi zote za Dkt.Samia S katika kuijenga Tanzania kuelekea Taifa lenye amani,utulivu ,Ustawi wa Maendeleo endelevu ya Kiuchumi,kijamii na kisiasa .
“Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Ilala tumeazimia kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 Wanawake wote wa wilaya ya Ilala tunamuunga mkono mwanamke mwezetu na kutangaza kwa nguvu zetu zote na kueneza mafanikio yote yaliopatikana chini ya uongozi wake”amesema Rehema.
Aidha Mwenyekiti Sanga amesema wanajipanga kujidhatiti kwenda kuhamasisha Wajasiriamali wenzao na kupita nyumba kwa nyumba kuwashawishi Watanzania wote wamuunge mkono kumpigia kura Rais ifikapo October 2025.
“Sisi Wanawake wa Wilaya ya Ilala wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi tutahakikisha kwamba Dkt.Samia Suluhu Hassan anapata kura kwa kishindo ili aendelee kuliongoza Taifa letu kwa kipindi kingine cha miaka mitano wanavuka na Mama Samia ,tunaenda na Mama Samia “amesema




More Stories
Aweso:Rais Samia ameweza kumtua mwanamke ndoo kichwani
TPTC kuendelea kuendesha kozi ya ulinzi wa amani kwa Watanzania
WMA yafikia asilimia 96 utekelezaji mpango kazi wa Mwaka