January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake wakicheza wakati wa mafunzo ya unyonyeshaji na makuzi kwa watoto wenye umri chini ya miezi sita yaliyoandaliwa na mradi wa USAID Tulonge afya katika Halmashauri ya Nyamagana jijini Mwanza jana. Mpigapicha Wetu

Jukwaa la Naweza latoa elimu kuhusiana na utapiamlo

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online,Mwanza

IWAPO mama ataanza kumpatia vyakula mtoto ambaye hajafikisha miezi sita anaweza kumsababishia magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na utapiamlo na kuharibu mfumo mzima wa makuzi yake hivyo ni vyema kuzingatia maelekezo na makuzi ya mtoto.

Wanawake wakicheza wakati wa mafunzo ya unyonyeshaji na makuzi kwa watoto wenye umri chini ya miezi sita yaliyoandaliwa na mradi wa USAID Tulonge afya katika Halmashauri ya Nyamagana jijini Mwanza jana. Mpigapicha Wetu

Pia,watoto wanapoumwa au kuonyesha dalili za kuumwa wazazi wanapaswa kuwakimbiza hospitalini badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji ambao huweza kuharibu mfumo wa makuzi yao.

Hayo yamebainishwa na wataalaamu wakati wa kongamano la afya ya mama na mtoto lilioandaliwa na Mradi wa Usaid Tulonge Afya kwa ajili ya kuwapatia elimu makuzi ya watoto wanawake wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza jana.

Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bertha Yohana amesema kumekuwapo na changamoto ya afya ya makuzi ya watoto kutokana na mila, tabia na desturi za jamii kushindwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu.

“Tumekuwa na tabia kwenye jamii wanafundishana wao kwa wao, wapo wanaoamini kwamba mtoto akinyonya maziwa ya amma pekee hashibi, jambo hili sio kweli, mtoto anaweza kunyonya maziwa ya mama akashiba bila kula chakula kingine mpaka afikishe miezi sita,” amesema

Amesema wakati mwanamke anapokuwa ananyonyesha mtoto mchanga anatakiwa asiwe na msongo wa mawazo, ale ashibe ili aweze kuzalisha maziwa ya kutosha.

Naye mhudumu ngazi ya jamii kata ya Mhandu, Rachael Mahulu alisema hakuna budi jamii ikaondokana na mila potofu za kuataka kuwalisha watoto wadogo vyakula na dawa kwa misingi ya kuwakuza kumbe kufanya hivyo wanawaharibu.

“Mtoto akiota meno haya yanaitwa ya plstikli, wengi wanawakimbiza kwa waganaga na kuwapaka dawa kienyeji, kufanmya hivi ni kosa nenda hospitali utapewa mwongozo,” amesema

Amesema iwapo mama akimnyonyesha mtoto wake mara kwa mara anamjengea uhusiano mzuri kati yake na yeye katika makuzi.

Naye Ofisa Uwanda (field officer),kutoka mradi wa USAID Tulonge afya wilaya ya Nyamgana, Esuphvat Lewis, alisema katika kongamano hilo wamefundisha tabia nne za kiafya katika makuzi ya mtoto ambayo ni pamoja na unyonyeshaji wa maziwa kwa kipindi cha miezi sita.

Zingine ni kuhakikisha mama analala na mtoto kwenye chandarua kimoja angalau mpaka afikishe miezi tisa, mama akiona dalili zozote hatarishi ampeleke mtoto hospitalini na njia za uzazi wa mpango baada ya mtoto kufikisha miezi 24.

Amesema katika mafunzo hayo jumla ya wanawake 50 wameshiriki kutoka kata za wilaya ya Nyamagana.

Nao baadhi ya wanawake walioshiriki mafunzo hayo, Tatu Ramadhani na Ester Suleiman kwa nyakati tofauti wamesema mafunzo hayo yameweza kuwafungua na kutambua mambo muhimu katika makuzi ya mtoto ambayo walikuwa hawayajui awali.

“Nimejifunza unyonyeshaji wa mtoto na jinsi ya kumlinda na malaria, kiukweli kuna changmoto kubwa wanawake wengi wnashauriana kuwapa watoto uji hasa wa udaga kumbe unaweza kumsbaishia matatizo makubwa,” amesema Tatu mkazi wa Igoma.

Mradi huu ambao unafahamika kama Mothers Meets Up events unafanyika kati ya wilaya 27 za Tanzania ambapo kupitia majukwaa ya watu wazima ya Naweza chini ya mradi wa Tulonge afya Tanzania kwa lengo la kuhamasisha huduma bora za afya kwa ngazi ya familia na jamii kwa kuondoa Mila pitiful na kuwapata mbinu za kiafya kujikinga na maradhi kama ukimwi , malaria, uzazi wa mpango na afya ya uzazi pamoja na ugonjwa wa kifua kikuu.