Na Heri Shaaban( Ilala)
SHULE ya Sekondari ya Serikali Juhudi iliyopo Gongolamboto wilaya ya Ilala, inajivunia mafanikio kitaaluma kwa miaka mitatu matokeo ya kidato cha sita matokeo ya Taifa (NECTA )imefaulisha kwa asilimia 100 kuanzia mwaka 2022 mpaka 2024.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa shule hiyo Happynes Pallangyo ,wakati wa Mahafari ya nane ya kidato cha sita ambapo jumla ya wanafunzi 343 walikabidhiwa vyeti vyao wanatarajia kufanya mitihani yao Mei mwaka huu .
“Shule yetu ya Juhudi kwa kipindi cha miaka mitatu Takwimu za kitaaluma matokeo ya kidato cha sita wanafunzi ufaulu asilimia 100 mwaka,2022 wanafunzi 200 walifanya mtihani kati yao wanafunzi 37 walipata daraja la kwanza 149 walipata daraja la pili na daraja la tatu walipata 16 mwaka 2023 wanafunzi 216 walifanya mtihani daraja kwanza 65 daraja la pili 118 na daraja la tatu 32” alisema Pallangyo.
Aidha alisema mwaka 2024 matokeo ya NECTA Taifa Division one wanafunzi 96 kati ya wanafunzi 270 waliofanya mtihani daraja la pili wanafunzi 148 na daraja la tatu wanafunzi 25 hayo ni mafanikio makubwa katika shule hiyo ambapo alisema wanapata ushirikiano mkubwa wa Wazazi Walimu na jitihada kuwasimamia wanafunzi.
Alisema wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu 2025 kwenye mitihani ya TAHOSSA waliweza kupata daraja la kwanza 147 daraja la pili 121 na daraja tatu 28 hapakuwa na daraja la nne wala 0 na mwaka huu wamepanga kuondoa daraja la tatu,daraja la nne na 0.
Akizungumzia shule hiyo alisema shule hiyo ipo Kata ya Gongolamboto Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam shule ya Serikali ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa na vyumba vinne na wanafunzi 90 wa kidato cha kwanza.
Alisema kwa sasa shule ina wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita ambapo jumla ya wanafunzi 4333 kati yao wavulana 2036 na wasichana 2297 na Alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais kwa utekelezaji wa Ilani ya chama vizuri ambapo katika sekta ya elimu Rais amefanya mambo makubwa na hivi karibuni Juhudi wanajenga shule ya sekondari ya kisasa ya golofa hayo ni maendeleo makubwa katika nchi yetu hasa sekta ya Elimu.
More Stories
Wasira afanya mazungumzo na Spika wa Jamhuri ya Cuba
Tanzania,Oman kushirikiana sekta ya Maliasili na Utalii
Dkt. Biteko: Serikali kujenga mtandao mkubwa mabomba ya gesi