December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jogging zatakiwa kuhamasisha utunzaji mazingira

Na Mwandishi wetu,Timesmajira,Online

WITO umetolewa kwa vijana   nchini  wametakiwa kutumia vikundi vya kukimbia mbio fupi (Jogging) kuhamasisha jamiii juu ya utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti ya kivuli na matunda.

Akizungumza hayo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam na Diwani wa Kata ya Buguruni ambae pia ni Katibu wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji hilo, Busoro Pazi wakati akizindua kampeni ya Boresha Afya Safisha Tunza  Mazingira na upandaji wa miti amesema ni vema vijana wanapofanya mazoezi kujua kuwa wanaweza kutumia muda huo katika kuweka mazingira safi.

Amesema jamii ikitambua namna gani wanaweza kuratibu  takataka itasaidia kwa kiasi kikubwa utunzwaji wa mazingira kuanzia majumbani hadi mitaani huku watu kuacha kutupa hovyo.

Amesema bado kunachangamoto kubwa katika jamii juu ya utunzaji wa mazingira kwani watu wamekuwa wakinywa maji na kutupa chupa ovyo au karatasi .

“Jamii ikielimika na kujua  takataka hizi  zinaweza kutumika kurejeleza katika matumizi mbalimbali katika jamii kama fursa na biashara,”amesema na kuongeza

“Kutokana na kukosa elimu katika jamii utakuta mtu anakusanya taka zote  sehemu moja badala ya kuzitenganisha hivyo kupitia mradi huu tumejifunza takataka hazitakiwi kukaa sehemu moja na kila takataka zinapozalishwa inatakiwa kutengwa kulingana na makundi yake,”amesema

Aidha amesema zipo takataka aina nyingi zipo zinazooza ambazo ni za vyakula na takataka za Chupa na hatarishi zikitengwa inakuwa rahisi kuzirudisha katika matumizi mbalimbali kama mbolea.

“Ulimwengu wa sasa unahitaji vijana kwenda na wakati, tunaelewa mazoezi ni afya lakini pia wanaweza kutumia umoja wao kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kutunza mazingira, ikiwemo kupanda miti pamoja na kuwa wabunifu katika vikundi vyao”amesema Pazi.

Aidha, ameupongeza uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa chini ya Mwenyekiti wake, Maliyatabu Shaaban kwa ubunifu waliouonesha wa kuanzisha kituo cha kuchakata taka na kuzipa thamani, Sambamba na kutoa ajira kwa vijana.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa,Maliyatabu Shaaban amesema kuwa, kuanzishwa kwa kituo cha kuchakata taka kichopo chini ya Taasisi ya nipe fagio katika Mtaa huo  kinakwenda kuleta mabadiliko katika suala la usafi wa mazingira ndani ya mtaa na Kata kwa ujumla.

“Leo tumezindua kampeni ya Boresha Afya Safisha, Tunza Mazingira pamoja na kampeni ya upandaji wa miti ya kivuli na matunda ndani ya mtaa wa Bonyokwa kwa kushirikiana wadau mbalimbali ambao wametuunga mkono, hii imetokana kuwa tunambolea ya kutosha ya kuweza kupandia miti hii kutoka kwenye kituo cha kuchakata taka”amesema Maliyatabu

Aidha, amesema licha ya kuzindua kampeni hizo, lakini pia wameweza  kufanya mazoezi ya kukimbia kutoka viwanja vya benki hadi kituo cha kuchataka taka kwa lengo la kujikinga na uviko 19, sambamba na kuokota taka za plastiki ngumu na mifuko ya laini na kuzipeleka kituoni hapo kwa ajili ya kupewa thamani ikiwemo chupa za plastiki kupelekwa kiwandani kwa ajili ya matumizi mengine na ambazo hazifai zinapelekwa dampo.

“Mfumo huu wa kuchakata taka sifuri, umekua rafiki sana kwa wananchi kwani mwanzo tulikua na dampo ambalo sio rafiki kwetu, lakini kuanzishwa kwa kituo hichi tunakwenda kubadilisha mazingira yetu yatakua Safi, na tutapanda miti kwa wingi kwa sababu tunambolea ya kutosha, taka tulizoziokota leo tumezileta hapa ili ziweze kuchakatwa”amesema Maliyatabu.

Naye, Muasisi wa Taasisi ya Jielimishe kwanza   ambayo inajishughulisha na jamii kwenye ulinzi wa kutunza mazingira, Henry Kazula amesema  kampeni ya Eco Jogging Club Tanzania (mbio za pole pole) ni kampeni ambayo inahamasisha ufanyaji wa usafi

“Tumeona kutumia vikundi vya wakimbiaji wa mbio fupi zitasaidia kufanya usafi katika maeneo wanayokimbia, leo tulikua na vikundi viwili, Corona Jogging na Canada, kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa tumeweza kuwa na washiriki wasiopungua 150 ambao wameweza kushiriki katika tukio hilo na kufanya usafi kwa umbali wa kilometer nne,”alisemaAlisema katika zoezi hilo wameweza   kukusanya taka takribani viroba 15 na kuzipeleka kituo cha kuchakata taka,kupitia mbio hizo zitasaidia utunzaji wa mazingirakaga,”amesema