January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Joe Biden: Trump ameiweka Marekani gizani kwa muda mrefu

Joe Biden amesema  Rais wa Marekani Donald Trump ”ameiweka Marekani kwenye giza kwa muda mrefu” alipozungumza wakati akikubali kuteuliwa kwake kupeperusha bendera ya chama cha Democratic kuelekea Ikulu mwaka huu.

Makamu wa rais wa zamani amesema  Trump  amesababisha ” hasira nyingi, uoga mwingi na mgawanyiko mkubwa kwenye  kazi ya kisiasa iliyochukua karibu nusu karne’’, ambapo kwenye kampeni za uchaguzi mkuu akiwa anaongoza kwa kura za maoni dhidi ya Rais Trump

Zimebaki  siku 75 kabla ya uchaguzi, Rais wa Republican ana muda mwingi wa kupunguza tofauti ya kura hizo.

Akiongea kwenye hafla mjini Wilmington, Delaware, Biden, 77 amesema ”sasa hivi ninawaahidi, ikiwa mnaniamini kwa kunipa jukumu hili la urais, nitahakikisha sisi tunakuwa bora zaidi, nitakuwa mshirika wa nuru, na si giza’’.

”Ni wakati wetu, wa kuwa pamoja na kuhakikisha hatufanyi makosa, kwa kuungana tunaweza na tutapambana na msimu huu wa giza Marekani,

Tutachagua matumaini dhidi ya hofu, uhalisia kuliko mambo ya kufikirika, haki kuliko upendeleo.”

”Tunaweza kuchagua njia ya kuwa na hasira zaidi, isiyo na matumaini, iliyogawanyika zaidi,” amesema Biden.

”Au, tunaweza kuchagua njia tofauti na wote kwa pamoja tukatumia fursa hii ili kupona, kufanya mabadilik kwa  kuungana”.

”Huu ni uchaguzi wa kubadili Maisha, hii itatupa mwanga wa namna Marekani itakavyokuwa kwa muda mrefu.”

Ameeleza  ” Tunachokijua kuhusu rais huyu ni kuwa ikiwa atapatiwa miaka mingine minne, atakuwa jinsi alivyokuwa miaka minne iiyopita’’.

”Rais ambaye hawajibiki, ambaye anakataa kuongoza, anayewalaumu wengine, anawafunika madikteta na kuchochea miale ya chuki na mgawanyiko.

”Je hii ni Marekani mnayoitaka kwa ajili yenu, familia zenu na watoto wenu?”

Wazungumzaji waliozungumza kwenye mkutano siku tatu zilizopita wamemkosoa Trump kuwa mtu asiyemudu kazi yake, mbinafsi, na hatari wa demokrasia.