November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT yakanusha uvumi kunyanyasa vijana

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limekanusha habari za uvumi ulionea kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinalenga kulichafua Jeshi hilo kwa kuonyesha picha zinazoashiria kunyanyawa kwa vijana hususan wa kike.

Kufuatia uvumi huo Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele amewatoa hofu wazazi,walezi na vijana kwa kusema taarifa hizo siyo sahihi huku akiwasihi vijana waendelee kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa.

Akizungumza Juni 2,2023 na waandishi wa habari Makao Makuu ya JKT mkoani Dodoma ,Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema,JKT kwa kushirikiana na mamlaka nyingine watachukua hatua kwa waliohusika kutokana na kulichafua Jeshi hilo.

“Kumekuwa na uvumi wa namna hii kila mwaka tunapoita vijana hasa wa mujibu wa sheria unaoashiria JKT kuna manyanyaso,hii siyo kweli taarifa hizo zipuuzwe.”amesema Brigedia Jenertali Hassan Mabena na kuongeza kuwa

“JKT limekuwa likichukua vijana wa mujibu wa sheria kila mwaka na wale wa kujitolea kwa lengo la kuwapa vijana mafunzo yaliyoandaliwa ili kuwajenga uzalendo,ukakamavu na kuwajengea ari ya kulilinda Taifa lao kwa nguvu zao zote .”

Amesema,JKT ndiyo sehemu salama ya kuwafanya vijana wafuate utamaduni wao badala ya kufuata tamaduni za nchi nyingine kupitia utandawazi.

Aidha amesema kuwa katika kuhakikisha mafunzo hayo yanawafikia walengwa JKT limeweka utaratibu mzuri na kila kamba linamlezi mwanamke (Matron) na mlezi mwanaume (Patron) ambao wanakuwa nao karibu wawapo kambini.

Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Mabena inapobainika kuna mkufunzi ambaye ameenda kinyume na taratibu za mafunzo hayo ,hatua kali zimekuwa zikichukuliwa dhidi ya wahusika ikiwemo kuondolewa kwenye ukufunzi.