Na Ashura Jumapili, Timesmajira Online, Kagera
Timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT QUEEN’S )wameshauriwa kuwapa mbinu wachezaji wa kiume katika mchezo huo wanazotumia katika mashindano na kuibuka kidedea ili na wao walete makombe Tanzania.
Ushauri huo umetolewa Projestus Rubanzibwa kwa niaba Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakati wa mapokezi ya timu hiyo ikitokea nchini Uganda ilikokwenda kushiriki mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA ) na kuibuka na ushindi wa goli 5-4 dhidi ya CBE kutoka nchini Ethiopia mchezo ulitimua vumbu uwanja wa Njeru uliopo nchini Uganda.
Rubanzibwa ,amesema timu hiyo iliweka kambi mkoani Kagera wakati wa maandalizi ya kuelekea mashindano hayo na walikuwa wanafanya mazoezi katika uwanja wa Kaitaba.
“Tuliwaasa,tukawatia moyo na kuwapa hamasa ya kutosha ili waweze kurejea na ushindi na hatimaye wamefanikiwa,”amesema Rubanzibwa.
Kocha wa JKT QUEEN’S Ester Chabuluma amesema katika mashindano hayo wamepata ushirikiano wa kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda kwa kuwandaa watanzania waliopo katika nchi hiyo kuwapa hamasa wachezaji ili waweze kupata ushindi ambao wamefanikiwa kupata.
Chabuluma,amesema walipofika mkoani Kagera kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo walipokelewa vizuri na wananchi na walipoondoka waliwahaidi kuleta ushindi ndio maana wamefika kuwaonesha kombe walilopata.
Amesema wanaenda kujipanga kuendelea na mashindano mengine ya Afrika ili waweze kupata ushindi.
Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo Annastazia Katunzi ,amewashukuru wananchi wa Kagera kwa kujitokeza kwa wingi kuwapokea.
“Sina cha kusema nawashukuru sana kwa sapoti yenu kwetu tunahaidi kuendelea kufanya vizuri,“amesema Katunzi.
Hata hivyo katika mashindano hayo timu hiyo imetoka golikipa bora ambaye ni Najiath Athuman,mchezaji bora Stumai Abdallah.
Hata hivyo mamia ya wakazi wa Manispaa ya Bukoba wamejitokeza kwa wingi kuipokea timu hiyo katika mji wa Rwamishenya licha mvua kunyesha lakini hawakukata tamaa waliendelea kuwasubiria wachezaji hao kwa hamasa kubwa.
JKT QUEEN’S wameibuka kidedea na kutwaa kombe la CECAFA baada ya kuwazidi wapinzani wao kutoka CBE ya Ethipia kwa mikwaju ya penati kwa goli 5 kwa 4.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship