November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT Marathon 2023 kutimua vumbi Juni 25

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetambulisha vifaa vya michezo vitakavyotumika katika mbio za JKT 2023 zinazotarajiwa kufanyika Juni 25 mwaka huu katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais mstaafu  wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete.

Akizungumza wakati wa kutambulisha vifaa hivyo Mkurugenzi wa Elimu,Utamaduni na Michezo wa JKT  Kanali Erasmus Bwegoge amesema mbio hizo ni miongoni mwa shughuli zinazotarajiwa kufanyika kuelekea kilele Cha maadhimisho ya miaka 60 ya JKT tangu kuanziashwa kwake huku akitaja viifaa vilivyozinduliwa kuwa ni pamoja na T-shirt ,medali,alama za mkononi na namba ambavyo vyote vitatumika katika mbio hizo.

Aidha amesema katika mbio hizo kutakuwa na mbio za kilometa Tano,10 na 21.1 huku akisema Kila mbio itakuwa na barabara zake za kupita ambapo wote wataanzia viwanja vya Jamhuri na kuishia katika viwanja hivyo.

Kanali Bwegoge amesema vituo vya kuchukulia vifaa ni pamoja na Royal Village na Bunge jijini Dodoma huku kwa nje ya Dodoma kituo kitakuwa Mlimani City na kwamba vifaa vitatolewa kuanzia Juni 17 -23 mwaka huu.

Ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi waendelee kujitoleza kwa ajili ya kujiandikisha Ili waweze kushiriki katika mbio hizo.

Ametaja zawadi za washindi amesema kwa mbio ndefu mshindo wa kwanza ataondoka na kitita sh.1 milioni na kuanzia mshindo wa sita Hadi wa kumi watajinyakulia kiais Cha sh.100,000.ambapo kwa kilometa 10 mshindo wa kwanza atajinyakulia kitita Cha sh.500,000 huku mshindo wa sita Hadi wa kumi wakiondoka na shilingi 50,000