Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo, imefanikiwa kupata sokp la mahinidi ya njano yapatayo tani milioni moja za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) nchini Misri.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakati wa hafla ya kutia sahihi mikataba ya ushirikiano wa sekta ya kilimo na jeshi hilo tukio lilifanyika hivi karibuni katika Makao Makuu ya Jeshi, Wilaya ya Chamwino, Dodoma.
Kusaya amesema, “moja ya mambo tutakayoshirikiana na JKT ni kuwatafutia masoko ya mazao kabla na baada ya kuzalisha ili kuwa na uhakika wa kuuza”
Katibu Mkuu huyo amelitaka jeshi hilo kuanza haraka kulima zao hilo ili kukidhi mahitaji ya soko.
More Stories
TARURA Kilimanjaro yatimiza ahadi ya Rais Samia
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria
Wananchi wakubali yaishe Bangi kubaki historia Tarime