February 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKCI:Tiba Mkoba ya Dkt.Samia yawafikia watu 21,324


Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)imesema toka huduma za  tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la  Dkt.Samia Suluhu Hassan Outreach Services ianze imeshawafikia watu 21,324 ,watuwazima wakiwa 20,112 na watoto 1,212 katika mikoa 20 nchini waliofanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.

Huku wagonjwa wengine 689 walitibiwa kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa jijini hapa leo,Februari 26,2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt.Peter Kisenge wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  utekelezaji wa maendeleo ya hospitali katika miaka minne ya serikali ya awamu  ya sita.

Dkt.Kisengi amefafanua kuwa kati ya hao 8,873 watu wazima wakiwa 8,380 na watoto 493 walikutwa na matatizo mbalimbali ya moyo na kuanzishiwa matibabu.

“Wagonjwa 3,249 watu wazima 2,765 na watoto 484 walikutwa na matatizo yaliyohitaji matibabu ya kibingwa na kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.

“Wagonjwa hao walitoka katika nchi za Somalia, Malawi, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Watu wa Comoro , Msumbiji, Nigeria, Siera Leone, Zimbabwe, Zambia, Uganda, Congo, Ethiopia, Burundi na wengine kutoka nje ya Afrika zikiwemo nchi za Armenia, China, Ujerumani, India, Norway, Ufaransa na Uingereza.

“Wataalamu wetu walivuka mipaka ya nchi na kwenda kutoa huduma za matibabu ya moyo katika nchi za Malawi, Zambia na Jamhuri ya Watu wa Comoro wakiwa katika nchi hizo walitibu wagonjwa 1,189 watu wazima walikuwa 851 na watoto 338. Wagonjwa 262 walipewa rufaa ya kuja kutibiwa JKCI.”ameeleza Mkurugenzi Kisenge.

“Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua na kubadilishwa Valvu za moyo moja hadi tatu, upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu ya moyo (Coronary Artery Bypass Graft Surgery –CABG), upasuaji wa mishipa ya damu na mapafu walikuwa 2,784 kati ya hao watu wazima walikuwa 1,880 na watoto 904.”amesema.
Mwisho.

Vilevile ameeleza kuwa kuwa serikali ilitoa Shilingi bilioni 2.16  kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya watoto mahututi na chumba cha wagonjwa mahututi cha watu wazima, ukarabati na utanuzi wa ICU ya watoto ambayo hapo awali ilikuwa na vitanda nane na hivi sasa inavitanda 16 na ICU ya wakubwa ambayo imetanuliwa na kuwa na vitanda kumi kutoka nane ambapo shilingi 503,450,051 zilitumika katika ukarabati huo.

Ameeleza kuwa Shilingi 1,465,683,469 zilitumika kununua vifaa tiba, shilingi 170,000,000 zilitumika kwa ajili ya tiba mtandao (Telemedicine) na shilingi 28,340,000 zilitumika kugharamia mafunzo ya wataalamu wa fani ya radiolojia na huduma za wagonjwa mahututi.

Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeajiri wafanyakazi wapya 186 wa kada mbalimbali, wafanyakazi 366 wamepandishwa vyeo katika madaraja mbalimbali. Taasisi iliwaongezea ujuzi wa kazi wafanyakazi kwa kuwapeleka kozi na muda mfupi watumishi 184, waliomaliza masomo ya kozi za muda mrefu ni 45 na waliopo masomoni ni  51.

Pamoja na hayo Dkt.Kisenge amesema kuwa Taasisi hiyo ni kati ya hospiatli mahili barani Afrika,inayofanya matibabu ya ubadilishadi wa valvu ya moyo bila kufungua kifua