Na Mwandhishi Wetu TimesMajira Online
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne ambaye pia ni shabiki mkubwa wa klabu ya Yanga, Dkt Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Wiki ya Mwananchi.
Katika maadhimisho hayo yatakayofikia kilele Agosti 30, timu ya Yanga itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Aigle Noir ya nchini Burundi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa.
Mbali na mchezo huo kuwa wa kifariki lakini pia utatumiwa na benchi la ufundi kuangalia maeneo yenye mapungufu ili kuyarekebisha haraka kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema, Dkt. Kikwete atawaongoza wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga kushuhudia matukio muhimu ya ambalo pia litatumika kutambulisha wachezaji wao wapya na wazamani watakaokuwa nao msimu ujao.
“Kama ambavyo inafahamika Agosti 30 ndio kilele cha Wiki ya Mwananchi na tutajumuika na Mwanayanga mwezetu Dkt. Kikwete, ambaye atatuongoza katika matukio ya kilele Cha Wiki ya Mwananchi,” amesemaBumbuli.
Pia amewataka mashabiki kuendelea kununua tiketi katika vituo mbalimbali vilivyotangzwa kwa ajili ya sherehe za Wiki ya Mwananchi zinazotarajiwa kupambwa pia na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na Harmonize, Chege, Madee, BillNass, Mzee wa Bwax, G Nako na wengine wengi.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania