January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jimmy Butler

Jimmy Butler apiga alama 40 kuiua Lakers

LAKE BUENA VISTA, Florida

TIMU ya Miami Heat imeibuka na Ushindi wa vikapu 115-104 dhidi ya Los Angeles Lakers katika mchezo wa 3 fainali ya Ligi Kuu ya kikapu Marekani (NBA). uliofnyika mwishoni mwa wiki.

Katika mchezo huo nyota wa Heat, Jimmy Butler ameifungia timu yake alama 40, rebounds 11 na assists 13 kuhakikisha timu yake inaibuka na ushindi.

Akizungumza mara baada ya ushindi huo kocha wa Heat Erik Spoelstra amesema, amefurahi tiu yke kuibuka na ushindi katika mcheo wa tatu finali ya NBA.

“Ninafurahi tumeshinda, wachezaji weangu walicheza kwa kujiamini, hivyo imani yangu michezo ijyo tutafanya vizuri zaidi ili tuwe mabingwa wa NBA, msimu huu,” amesema Spoelstra.