June 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jiji la  Dar-es-Salaam latenga bilioni 18 za mkopo wa asilimia 10 

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online -Ilala

Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imetenga kiasi  cha bilioni 18,kwa ajili ya  mkopo wa asilimia 10, inayotolewa  kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo,katika kongamano la Jukwaa   la   Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wa  Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam, amesema fedha hizo zitakopeshwa kwa vikundi vya wajasiriamali vilivyosajiliwa na kutimiza taratibu za kukopa vilivyopo wilayani Ilala.

Mpogolo, amesema jumla ya vikundi 940 mpaka sasa vimeishaomba mkopo huo wa asilimia 10, hivyo halmashauri hiyo imejipanga kuanza kutoa fedha hizo.

Pia amewataka wajasiriamali wadogo  wa wilaya hiyo kukaa mkao wa kupokea fedha kupitia taasisi za benki ambazo zimepewa jukumu la kuwakopesha.

“Vikundi vyote vilivyotimiza taratibu kutoka Jimbo la Segerea, Ilala na  Ukonga vyote vitapewa fedha, ili kukuza uchumi wa nchi yetu,”.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam,Elihuruma Maberya,amesema utaratibu wa mikopo kwa sasa ngazi ya Halmashauri wanatoa benki na kabla ya kukopa lazima wakuhakiki.