December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la Polisi Tanzania kesho kuteketeza Silaha haramu

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, (Polisi )

Jeshi la Polisi Nchini linatarajia kuteketeza Silaha zote haramu zilizosalimishwa katika Kampeni Maalum iliyofanyika nchi nzima

Akizungumza na Waandishi wa habari msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini David Misime alisema zoezi hilo la kusalimisha Silaha nchini lilianza Septemba mosi mpaka Octoba 31 mwaka huu.

” Kampeni ya kusalimisha Silaha ilizinduliwa rasmi Septemba 9 mwaka huu Viwanja vya mashuja Dodoma na Naibu waziri wa Mambo ya Ndani nchini baada Tangazo la SERIKALI wa Msamaha wa usalimishaji wa Silaha kwa hiari Namba. 537 tarehe la Agosti 26 mwaka 2022 ambalo lilieleza kwa yeyote anayemiliki Silaha kinyume cha Sheria anatakiwa kusalimisha ” alisema Misime .

Misime alisema kwa mujibu wa taratibu na miongozo mwezi wa usalimishaji wa Silaha haramu Afrika ,baada ya zoezi la usalimishaji Silaha kukamilika zinatakiwa kuteketezwa kwa Moto hadharani na Wananchi washuhudie ikifanyika hivyo .

Alisema zoezi hilo litafanyika asubuhi Viwanja vya Shabaha vya Jeshi la Polisi vilivyopo Kunduchi Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Jumanne Sagini .

Aidha Jeshi la Polisi linawaalika viongozi wa Serikali za mitaa na Wananchi kuhudhuria na kujionea mafanikio makubwa aliopatikana kutokana na kampeni hiyo .