Judith Ferdinand,Mwanza
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limesema halitasita kuwachukulia hatua wahalifu wote wanaojichukulia sheria mkononi ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Hayo yamesema na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi,
wakati wa hafla ya kuwatunuku zawadi na vyeti baadhi ya askari walioshiriki operesheni ya kuwakamata watuhumiwa wa mauaji ya wanawake watatu waliouawa kwa kukatwa mapanga na kisha miili yao kutupwa kwenye mto wilayani Ilemela usiku wa kuamakia Januari 19 mwaka huu.
Ng’anzi amesema jeshi hilo lipo tayari kuwatumikia wananchi kwa moyo uliotukuka na watafanya kazi kwa kuhakikisha raia na mali zao zinakuwa salama.
Ambapo ametoa tahadhari kwa wahalifu kuwa Mwanza hawana nafasi wataingia lakini hawatatoka salama huku akiwahakikishia wananchi kuwa jeshi limejipanga kutokomeza uhalifu wa aina yoyote.
Amesema watafanya kazi muda wote kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Mwanza na kipaumbele chao ni kuona matukio yote ya uharifu hayatokei iwe ni nchi kavu, majini au angani.
“Mahali popote polisi watafika na kiapo chetu ni kilekile kuwa hatutamuonea mtu wala kumpendelea mtu,” amesema Ng’anzi.
Akizungumza baada ya kukabidhi vyeti hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel,Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Massala,amesema uongozi wa Mkoa uko tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ambao utahitaji.
Masalla amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwabaini wahalifu kwani anatambua jitihada kubwa zinazofanywa na jeshi hilo katika kuwalinda raia wake huku akiwatoa hofu watu wanaotaka kuwekeza katika Mkoa huo kuwa upo salama kwani ulinzi na usalama umeimarishwa.
Wakizungumza kwenye hafla hiyo baadhi ya watetezi wa haki za binadamu na viongozi wa dini akiwemo Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke amesema njia pekee inayoweza kubadirisha mtazamo wa raia ,kupunguza matukio ya mauaji na kuimarisha hali ya amani nchini ni pamoja na jamii kuwa na hofu ya Mungu.
Hivyo aliviomba vyombo vya habari vitoe nafasi kwa viongozi wa dini ili waweze kutoa elimu na kuzifinyanga nafsi ili ziachane na imani potofu na warejee kwa Mungu wao.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa