December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la Polisi lafanikiwa kukamata mifugo 319, iliyoibiwa

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online ARUSHA

Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo Nchini limesema kuwa katika kipindi cha mwezi juni mwaka huu limefanikiwa kukamata mifugo 319 iliyokuwa imeibiwa maeneo mbalimbali hapa Nchini.

Akitoa taarifa hiyo leo Juni 16,2023 alipotembelea mnada wa kikatiti wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini kamishina msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua amesema watuhumiwa 153 walikamatwa na tayari wamefikishwa mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.

Kamanda Pasua amebainisha kuwa kikosi hicho kwa kushirikiana na wananchi wameunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kutokomeza wizi wa mifugo ambapo amebainisha kuwa wakaguzi kata waliopo katika maeneo mbalimbali hapa Nchini wamendelea kutoa elimu na kuwashauri wananchi kutokuwaacha watoto wadogo kuchunga mifugo.

Kwa upande wake Bw.Wilson Shami amelishukuru Jeshi la Polisi Nchini kwa namna ambavyo wamembana na uhalifu wa mifugo hapa Nchini kitengo kilichopelekea kupungua kwa idadi ya wizi wa mifugo katika maeneo mbalimbali hapa Nchini, ameongeza kuwa kitendo cha kuweka askari kata katika maeneo yao kimesadia sana kuweka nidhamu kwa wale wote wenyenia ya kuiba mifugo.

Kwa upande wake Jobard Thadeo ambae ni afisa mifugo wa halmashauri ya Meru amerishukuru Jeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo kwa namna ambavyo Jeshi hilo linavyoshirikiana nao katika kutoa elimu juu ya kusimamia mifugo yao ambapo amesema vikundi ambavyo vimeanzishwa vileta matokea mazuri katika kudhibiti uhalifu katika maeno yao.