January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la polisi Dar lawatoa hofu wananchi kuelekea Pasaka

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limetahadharisha wale wanaofikiria kufanya uhalifu siku ya Sikuu ya Pasaka waache mara Moja watashughulikiwa ipasavyo kwani Jeshi liko Imara kuhakikisha hali ya Usalama inakuwa shwari

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Kamanda wa Kanda Maalumu wa Dar es salaam SACP Jumanne Muliro amesema Polisi hawatasita Kufuatilia watu watakaotaka kupanga njama za kufanya uhalifu hawatalala kwani kila sikukuu kumekuwa na baadhi yao kutumia siku hivyo hivyo Jeshi litaendelea kufanya doria kila mahali.

Hata hivyo amewaomba Wazazi,Walezi siku ya sikukuu kuwa karibu na Watoto katika siku hiyo kwani kunakuwa na kupotea kwa watoto hivyo amewasihi ni bora wasiwaruhusu kwenda kwenye kumbi za starehe wakiwa wenyewe bora wawazuie

Aidha hali ya Usalama katika Kanda ya Dar es salaam ni shwari ikilinganishwa na miaka ya nyuma kulikuwa na matukio mbalimbali ikiwemo mtu kuprwa fedha akitokea benki na hawakamatwi wahalifu lakini saa hivi Jeshi halina budi kupongezwa kwa operesheni Kali inayofanyika kila siku chini ya Kamanda SAP Jumanne Muliro