LONDON, England
ALIYEKUWA nyota nambari tatu katika mchezo wa tenis duniani kwa upande wa wanaume Milos Raonic, amejiondoa kwenye mashindano ya tenis ya Wimbledon mwezi huu, kutokana na jeraha la ndama.
Raonic, mwenye umri wa miaka 30 raia wa Montenegro, mara ya mwisho alishiriki kwenye mashindano ya Miami Open Masters 1000 mnamo Machi akifungwa na Hubert Hurkacz katika hatua ya 16 bora kabla ya kukosa msimu mzima wa French Open.
“Nilitaka kushiriki lakini nina huzuni kubwa na ninaumia kwamba sitakuwa tayari kushindana Wimbledon mwaka huu,” nambari 18 ya ulimwengu Raonic amesema katika barua yake kupitia ukurasa wake wa Instagram mwishoni mwa Jumamosi.
Amesema, alikuwa akilenga kurudi kwa hatua katika uwanja wa nyasi lakini hakuweza kumaliza kabisa shida hiyo kwa wakati.
“Nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii kuiponya lakini nilikuwa na shida ndogo, Kwa hivyo sitakuwa tayari kwa Wimbledon. Nitafanya kazi kwa bidii ili kurudi haraka iwezekanavyo,” amesema Raonic.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania