Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
- Inaweza kulipwa kwa mwezi, miezi 4, miezi 6 au 12.
- Kiwango cha chini cha akiba ni Tshs 7,500
- Malipo ya fidia kwa bima ya maisha ni kwanzia Milioni 3.5 hadi Milioni 50
Elimu ndio zawadi kubwa na bora unayoweza kumpatia mtoto wako kuhakikisha anatumia fursa zote maishani.
Kwa kushiriana na kampuni ya bima ya Sanlam, benki ya NMB inatoa huduma ya bima ya elimu ili kuipa familia amani, wakati mmiliki wa bima atakapofariki, gharama ya masomo ya watoto italipwa na bima.
Bima hii ina sehemu kuu mbili;
- Kuweka Akiba
- Kinga ya maisha
Kwenye kuweka akiba, inafuata utaratibu wa kuweka kila mwezi kuanzia miaka 7 hadi miaka 18 na faida ya ziada ya bima ya maisha. Mmliki wa bima atakapofariki kabla ya mwisho wa mkataba, bima itaendelea kuwalipa wanufaika mpaka mwisho wa mkataba.
Kwenye kinga ya maisha, mmliki wa bima atakapofariki kabla ya mwisho wa mkataba, bima hii itawalipa fidia wanufaika tajwa wa mkataba huu kwa kiasi kilichochaguliwa katika mpango huu wa bima.
Endapo mwanachama hatofariki katika kipindi cha mkataba wa bima, bima hii itarejesha fedha ya bima ya maisha (fidia) kulingana na muda wa bima hiyo.
Vile vile, miaka mitano ya mwisho ya mkataba wa bima, mwanachama ataruhusiwa kutoa pesa kila mwaka mpaka mwisho wa mkataba.
Aidha, mteja anaruhusiwa kutoa fedha kidogo kwa kiwango kisichozidi asilimia 50 ya thamani ya mfuko.
Kwa mujibu wa NMB, Mwanachama ataendelea kupokea riba katika fedha iliyowekezwa kama akiba bila malipo ya ziada ya michango ya bima.
Unachohitaji kupata bima hii;
- Nakala ya kitambulisho halali chochote
- Leseni ya udereva
- Kitambulisho cha Taifa/ Paspoti
Tembelea tawi lolote la benki ya NMB kupata bima yako au piga simu namba 0800 002 002 bure!
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi