Na Penina Malundo, TimesMajira Online
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo,amewataka askari wapya kuhakikisha wanalinda nchi kwa uadilifu kwani ndio jukumu lao kubwa na wanatakiwa kuishi ndani ya kiapo chao.
Pia amewataka kuhakikisha wanaishi na kiapo chao na kuwa tayari kutekeleza majukumu hayo mahala popote bila kuchagua kwani jeshi ndio linajua wapi wanaweza kutumika.
Aidha alikipongeza Chuo cha Mafunzo ya Awali ya Kijeshi cha RTS Kihangaiko kutokana na usimamizi wa mafunzo na ujenzi wa miradi ya kujitegemea.
Jenerali Mabeyo amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa sherehe za kuapa kwa Askari wapya kundi la 39 katika chuo hicho kilichopo Msata Bagamoyo Mkoani Pwani.
Amesema hana Shaka na mazoezi waliyopatiwa askari hao, kwani ameshuhudia kupitia vyombo vya habari pindi walipokuwa wakihitimisha mafunzo ya Porini.
Amesema kufanya zoezi la pamoja kwa kujumuisha vikosi mbalimbali tena kwa kutumia gharama za shule ni hatua kubwa ya kupongezwa. Ameongeza kuwa anafurahi kuona askari wapya mbele yake kwani ni ishara kwamba wameiva na wako imara katika kutumikia JWTZ .
“Pongezi kubwa ni kwa wakufunzi waliohakikisha wanafika hatua hiyo ya kuwafanya askari wetu wameiva kimazoezi na kuwa imara,”amesema
katika hatua nyingine aliwataka watu wote wenye jambo au masuala na jeshi hilo kutozunguka wafuate utaratibu wa kijeshi badala kutaka kuwatumia viongozi wengine wakati mkuu wa majeshi na wasaidizi wake wapo.amesema
More Stories
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme