
Na Israel Mwaisaka, Sumbawanga
Mahakama ya mwanzo Ilemba Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa imewahukumu kifungo Cha miezi 6 vijana 7 kati ya 8 waliofikishwa katika mahakama hiyo kwa kosa la uzushi wa kuibiwa nyeti wakati siyo kweli.
Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo baada ya kumzushia Masanja Joseph Sen (34) mkazi wa Kijiji Cha Ilemba kuwa amewaibia nyeti ambapo walimvamia kumpiga na kumsababishia maumivu makali.
Mahakama hiyo chini ya Hakimu Rajabu Ukwaju iliwakuta na hatia watuhimiwa 7 kati ya 8 na kuwapa adhabu hiyo ya kifungo Cha miezi 6 jela na kulazimika kumlipa fidia ya Tshs,100,000 Kila mmoja kutokana na maumivu aliyoyapata.
Sambamba na hilo jeshi la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia Bosco John Fatachi (38) mkazi wa Kijiji Cha Kambo wilayani Kalambo kwa kosa la kumshambulia mtoto wa umri wa miaka 8 akimtuhumu kumuibia Pipi yenye thamani ya Tshs,200 dukani kwake.
Hakimu huyo amedai kuwa ametoa adhabu hiyo ili iwe ni fundisho kwa Watu wengine Wenye tabia za uzushi kama huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Shadrack Masija ni kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kutenda kosa hilo alitoroka na jeshi hilo liliendelea kumtafuta hadi walipomkamata.
Amesema kuwa kwa Sasa wanaendelea na uchunguzi na kuwa ukikamilika watamfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

More Stories
Prof.Mbawara:TMA yakamilisha ufungaji wa mitambo miwili ya uangazi wa hali ya hewa
PBPA yapongezwa kwa usimamizi wa upatikanaji wa Mafuta nchini
Ujenzi wa Kituo cha Kupunguza Msukumo wa Mafuta Handeni wafikia asilimia 77