December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jay z avaa saa ya bilioni 7

NEW YORK, Marekani

NYOTA wa Hip Hop nchini Marekani, Shawn Corey Carter maarufu kama ‘Jay-Z’ ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuonekana akiwa amevaa saa yenye thamani ya Dolla milioni 3, ambayo kwa pesa ya Tanzania ni Bilioni 7.

Jay-Z, alionekana akiwa na saa hiyo mwishoni mwa wiki katika sherehe ya mfanyabiashara aitwae Michael Rubin.

Katika sherehe hiyo, nyota mastaa mbalimbali maarufu wamehudhulia, akiwemo Beyonce, Travis, na J Balvin Quavo.