December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wakazi wa Dar wakaribishwa kununua hisa

Na David John, TimesMajira Online

MENEJA mkuu wa Kampuni ya Jatu PLC  Mohamed Simbano, amewataka watanzania hususani wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza katika maeneo ili waweze kununua hisa kwenye kampuni hiyo.

Akizungumza Jijini humo leo, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni katika maeneo ya  vituo mbalimbali mkoani Dar es Salaam, hivyo wadau waendelee kununua hisa za Jatu Plc lakini pia unaweza kumnunulia na mtu mwingine.

“Kimsingi unapokuwa na hisa unapata faida na kupatiwa gawio la faida kila Mwaka  na pia hisa ni dhamana na mlango  wa kushiriki kilimo cha kisasa, ukinunua hisa unakuwa wakala wa bidhaa za Jatu na zaidi unapata mikopo yenye riba nafuu kutoka Jatu Saccos,” amesema Simbano.

Simbano ameongeza kuwa, Jatu imelenga kuleta Mapinduzi chanya katika sekta ya kilimo na matarajio yake kuona kila mtu anafaidika zaidi kwa kununua hisa za Jatu .Kwa kupitia kauli mbiu ya Buku tano inatosha.

Amesema, kama kweli watanzania wanataka kuondokana na umasikini ni vyema wanatumia fursa hiyo kuinua kipato chao kwa kununua hisa ambazo zitawafanya kupata gawio kutokana na faida atakayokuwa ameitengeneza.

Kampeni ya Jatu PLC inaendelea nchi nzima, hivyo watanzania popote watakapoona gari la Kampuni hiyo basi wachukuwe hatua na kununua hisa .ambayo pia itawafanya kuwa mwanafamilia wao.