Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka ameongoza viongozi mbali mbali, wadau wa maendeleo, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyoka kimkoa wilayani Kilosa.
Katika maadhimisho hayo DC Shaka alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kighoma Malima ambapo amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya majanga na maswahiba mbalimbali ambayo yanapelekea kuharibu utu wao mbele ya jamii sambamba na kuwakatisha tamaa katika kutimiza ndoto zao za baadae.
“Kauli mbiu ya mwaka huu ni Haki za mtoto , tulipotoka, tulipo tuendako ambayo inaitaka jamii kwa ujumla kufanya tafakuri ya kina juu ya upatikanaji wa haki za watoto tangu zilipoainishwa katika Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008″ amesema Shaka

Hata hivyo Dc Shaka ameendelea kutoa msisitizo juu kuwaelimisha na kuwakumbusha wazazi, walezi na watoa huduma wote wajibu wao katika kutekeleza haki tano za msingi za mtoto ambazi ni haki ya kuishi, haki ya kuendelezwa, haki ya kulindwa,hski ya kushiriki na haki ya kutobaguliwa.

“Niendelee kuwahakishia kuwa serkali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na kuweka mazingira rafiki na shirikisha itaendelea kuhakikidha haki nilizozianisha na ulinzi wa myoyo unapatokana katika ngazi zote” Amesisitiza Shaka.
More Stories
CHODAWU,ILO waungana kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani
HGWT yatoa wito jamii kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya ukatili
Tantrade yawaita wawekezaji wa ndani, nje kuwekeza uboreshaji wa uwanja wa maonesho Sabasaba