Na Joyce Kasiki,TimesMajira,Online,Dodoma
MKURUGENZI wa Huduma za Kinga,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi amewataka watendaji kuanzia ngazi za mashina kuhamsisha ujenzi wa vyoo na kuhakikisha kila mwananchi anatumia choo bora.
Dkt.Subi ametaja mikoa ambayo bado ipo chini kwa ujenzi na matumizi ya vyoo bora kuwa ni pamoja na Kigoma,Lindi,Dodoma na baadhi ya mikoa ya Kanda ya ziwa ambapo kwa baadhi ya mikoa vinara kwa vyoo bora ni pamoja na Dar es Salaam ,Iringa na Njombe.
Dkt.Subi ametoa kauli hiyo leo jijini hapa kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ,wakati akizungumzana waandishi wa habari kuhusu siku ya matumizi ya choo duniani ambayo huadhimishwa Novemba 9,ya kila mwaka.
Amesema lengo ya siku hiyo ni kuikumbusha jamii kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za afya ikiwa ni hatua muhimu ya kujikinga na maradhi yanayoenezwa kwa njia ya uchafu.
“Wiki ya Usafi wa Mazingira mojawapo ya mikakati mahususi ambayo inatumika kuibua na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa usafi katika ustawi wa jamii hasa katika Nyanja za Afya,elimu,maji na uchumi lakini pia siku hii ina lengo la kuikumbusha jamii kutumia vyoo bora ili kujikinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza yakiwemo ya kuhara,kuhara damu ,kipindupindu na magonjwa ya minyoo ,”amesema na kuongeza kuwa
“Choo bora ni kile ambacho kina ukuta,Mlango, sakafu inayoweza kusafishwa ,kilichoezekwa vizuri na chenye sehemu ya kupumulia hewa ili kuondoa harufu ndani ya choo,”amesema
Aidha amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Zingatia usafi wa jinsia kwa usafi wa mazingira endelevu ‘ni kauli mbiu ambayo inaongeza umuhimu wa ujenzi wa vyoo bora kwa jamii na maeneo yote yenye mikusanyiko pamoja na kuweka mazingira katika hali ya usafi wakati wote.
Amesema matumizi ya vyoo bora ni afua muhimu katika kukinga na kudhibiti maradhi ya kuambukiza huku akisema asilimia 40 ya magonjwa
yanayosababishwa na uchafu.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini