Na Zena Mohamed,TimesMajira Online-Dodoma
WAZIRI wa Nchi , Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira Seleman Jafo amezindua Mkakati wa Kitaifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya tabia nchi huku ikiitaka jamii kuishi kwa kufuata misingi ya ajenda za kimazingira.
Akiongea katika uzinduzi huo jijini hapa leo,kuelekea siku ya kilele cha wiki ya mazingira Duniani itakayoadhimishwa kesho Duniani kote ambapo kidunia hufanyika nchi Pakstan huku kitaifa yakifanyika Dodoma amesema, mkakati huo utasaidia kuondokana na uharibifu wa mazingira uliopo.
Amesema,kutokana na mapinduzi ya viwanda na shughuli za kibinadamu zimeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia nchi na kuipa changamoto Dunia katika kutafuta suluhu za kimazingira.
“Shughuli za binadamu kama vile kilimo,uchimbaji wa madini,uchomaji mkaa na ufugaji ni vyanzo vikubwa ambavyo huharibu mazingira,jamii inapaswa kwenda na wakati kwa kufuga kisasa, lakini pia kutumia nishati mbadala.
“Juhudi za kulinda na kuhifadhi mazingira zisiposhughulikiwa ipasavyo zitaleta athari na Dunia haitakuwa tena sehemu salama ya kuishi,”amesema Jafo.
Amefafanua zaidi kuwa, wataalamu wanasema asilimia moja ya pato la Taifa linapotea kila mwaka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. huku ikikadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wa ukanda wa pwani watakabiliwa na changamoto za Mazingira ifikapo mwaka 2030 ikiwa jamii haitaacha shughuli za kibinadamu zinazoathiri mazingira.
Pia ametaja athari moja wapo ambayo imetokana na Mabadiliko ya tabia nchi na kusema kuwa maji ya ziwa Tanganyika yameongezeka na kufikià mita mbili Jambo ambalo si salama kwa maisha ya binadamu.
“Tusiposimama pamoja Katika kutekekeza ajenda ya mazingira dunia yetu haitakuwa salama,wavuvi wanapaswa pia kuvua kwa kutumia zama zinazokibaliwa ili kulinda viumbe wa majini,”alisema.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best