Na Queen Lema,Timesmajira Online,Arusha
Serikali imeitaka jamii kuhakikisha kuwa wanalinda mazingira ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha watoto namna ya kutunza mazingira ili kukabaliana na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa sasa mabadilikonya tabia ya nchi hapa nchini yamesababish uwepo wa madhara ambayo yanawakumba watoto jambo ambalo nao wanatakiwa kuanza kuchukua hatua ili kulinda kizazi kijacho.
Hayo yameelezwa jijini Arusha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Suleman Jaffo wakati akiongea kwenye siku ya Watoto Duniani ambayo kwa Tanzania imeadhimishwa mkoani Arusha.
Jaffo amesema kuwa siku ya mtoto ni muhimu hasa kwenye suala zima la mazingira ambapo kwa sasa bado madhara ya mabadiliko ya tabia ya nchi yameendelea kuthiri jamii hasa kundi hilo.
Amesema kuwa mabadilko hayo ya tabia ya nchi yanaweza kuepukika endapo tu jamii itaungana kwa pamoja lakini pia kuwahusisha watoto kwa kuwa hata nao yana waathiri.
“Mjengee mtoto kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi hii itamfanya aweze kuwa balozi mzuri wa mazingira na hata athari zitapungua kwa kiwango kikubwa kwani zina waathiri hata wao,”.
Aidha amesema kuwa Serikali imejiwekeza katika kumsaidia mtoto kwani ana haki ya kuthaminiwa pamoja na kuendelezwa.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Amon Mpandu amesema kuwa watoto wana haki zao jamii inatakiwa ihakikishe kuwa zinafuatwa.
Amesema haki za watoto kama vile haki ya kuishi, haki ya kulindwa dhidi ya ukatili, kuendelezwa kielimu pamoja na kushirikishwa katika mambo mbalimbali katika jamii.
Awali watoto ambao walishiriki katika siku hiyo wamrsema kuwa pamoja na kuwa haki zao zinalindwa kwa kiwango kikubwa sana lakini jitihada kubwa dhidi ya mabadiliko tabianchi kwa kundi hilo zinaitajika kwa haraka.
Watoto hao wamedai kuwa wapo baadhi ya watoto ambao wanaongoza kwa kuharibu mazingira kwa kuwa hawana elimu thabiti ya mazingira hivyo ni muhimu kwa kila mzazi kuhakikisha anakuwa balozi ikiwezekana kila mtoto kupewa mti na sehemu ya kutunza ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Elke Wisch amesema watoto hawapaswi kuachwa nyuma kwenye mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwani wakiwezeshwa kutakuwa na kizazi kinachotunza na kuyalinda mazingira.
Maadhimisho ya siku ya watoto Duniani ni kumbukizi ya azimio la umoja wa mataifa juu ya haki za watoto lililofanyika mwaka 1989 na nchi wanachama walikubaliana kufanya maadhimisho hayo kila ifikapo November 20 kila mwaka.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi