January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Itel yatoa msaada shule ya msingi Ubungo Nhc

Na Mwandishi wetu,timesmajira

MENEJA Mahusiano wa Kampuni ya simu ya Itel nchini,Fernando Wolle amesema katika kutambua umuhimu wa sekta ya elimu nchini,Kampuni yao ya Itel imejipamba kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan  jitihada zake za kuhakikisha wanaisaidia  Serikali katika kuendeleza miundombinu ya elimu.


Pia kampuni hiyo,imeweza kutembelea Shule ya Msingi Ubungo NHC kwa lengo la kuwasaidia  watoto wanaotoka katika mazingira magumu ambazo zina vipato vya chini kwa kuwapatia  vifaa vya masomo.


Akizungumza  mwishoni mwa wiki katika zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo,Wolle amesema  wamekuwa wanaunga mkono jitihada za serikali kwa kutoa vifaa vya masomo ikiwa chini ya kampeni yao ya upendo wakati wote ambayo ilianzishwa mwaka 2003 ikilenga kurudisha fadhila kwa jamii kwa kuwasaidia wanafunzi au watoto kuwa na mazingira mazuri ya kusomea au vitendea kazi vya shuleni.


Amesema tayari Kampuni yao imefanya matukio mbalimbali yakurudisha fadhila kwa jamii katika shule na vituo vya watoto Yatima tangu mwaka 2016 mpaka sasa.
“Hakuna aside fahamu kuwa watoto ni hazina na ni taifa lijalo,hivyo sisi itek kwa kutumia kaulimbiu yetu ya Enjoy Better Life tunahakikisha tunatengeneza mazingira mazuri kwaajili ya kutimiza azma yetu ya kuwasaidia watoto kufurahi maisha bora,”amesema na kuongeza


“Programu hiyo kwa sasa inafanyika nchi zote za Afrika ambazo itel inapatikana,hivyo tumeona ni vema kutembelea shule ya Ubungo NHC na kusaidia watoto waliopo katika mazingira magumu,”amesema


Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni hiyo,Elizabeth Leiya amesema miongoni mwa vitu walivyowasaidia ni pamoja na  mabegi,madaftari, Kalamu,Chupaza maji na miamvuli kwa kipindi hiki cha mvua.”pamoja na msaada huo kwa watoto hawa tumeipa shule shelfu 20 za kuhifadhia vitabu pamoja na vitabu vya kiada 217 kwa masomo ya Sayansi, Hesabu na Kiingereza kwa darasa la tatu ,nne na la tano,”amesema
Aidha amesema  msaada huo kwa pamoja unathamani ya kiasi cha sh.milioni tano na zoezi hili litakuwa endelevu katika kuunga mkono jitihada za Serikali. 
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule Ubungo NHC,Paul Mdachi ameshukuru kampuni hiyo kwa hatua ya kuisaidia shule hiyo na kuiomba kuendelea kujitoa katika sekta y elimu kwani watoto wengi wanachangamoto.
“Tunashukuru kwa vifaa hivi kwani vitasaidia watoto wetu kusoma kwa moyo shuleni na kuchagua shule hii kutoa msaada mmewekeza hazina kubwa kwa vijana wetu na kupunguza kiasi kikubwa cha matatixo ya shule yetu,”amesisitiza Mwalaimu Mdachi
MwishoooÂ