Na Mwandishi wetu, timesmajira
KAMPUNI ya Simu ya mkononi Itel nchini inatarajia kuzindua simu mpya Itel A 60 itakayowarahisishia wateja wao katika matumizi ya Mtandao na kuendelea kuwaunganisha watanzania kidigitali.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari ,Afisa habari wa Kampuni ya Simu hiyo,Fernando Wolle amesema wameleta simu hiyo ambayo inaweza kutumiwa na watu wa kipato tofauti tofauti wakiwemo vijana wa vyuoni,mama lishe,machinga na watu wenye vipato vya chini ambao wangetamani kumiliki simu yenye uwezo bora zaidi katika matumizi.
Amesema simu hiyo ni simu yenye sifa ya kuwa na muonekano wenye kuvutia huku mteja ataweza chagua simu katika rangi tatu zinazokuja na simu .”Hii simu inasifa ya kuwa na bei nafuu kwenye soko katika kundi la simu zenye uwezo wa 4G na kioo kikubwa ambayo inaonyesha vizuri,”amesema na kuongeza
”Tunaleta simu hii kwa lengo la kuwafanya wateja wetu waweze kufurahia maisha ya kidigitali na ni muendelezo wa kuwaletea wateja wetu bidhaa nzuri kwa ajili ya matumizi ya internet,”amesema.
Aidha Wolle amesema kampuni hiyo imeazimia kuhakikisha kila mtanzania mwenye ndoto ya kumiliki simu janja yenye uwezo mkubwa na bajeti ndogo katika matumizi yake.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba