Na Penina Malundo ,Timesmajira
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah MMwandumbya amekitaka Chuo Cha Kodi (ITA) kuendelea kutoa mafunzo ya viwango vya juu kuzingatia kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani dunia ndipo inapoelekea kwa sasa.
Akitoa wito huo jana jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya kumi na saba kwenye chuo cha kodi (ITA) ambapo wamehitimu jumla ya wahitimu 417,Naibu Katibu huyo kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na chuo hicho kwenye kutoa mafunzo ya kodi na forodha kwani inachangia kuongeza makusanyo ya kodi kwenye Taifa.
Amesema chuo chao kinapaswa kujikita kufanya tafiti mbalimbali zitakazotoa changamoto kwenye mfumo wa ukusanyaji wa kodi huku mapendekezo mengi kwenye tafiti yanakosa utafiti kwenye jamii hivyo yataleta mapendekezo na tafiti kwenye kufikia malengo wanayoyataka.
“Chuo kinapaswa kujikita kufanya tafiti ili kuibua changamoto ambazo zitaweza kufanyiwa kazi katika kuleta mapendekezo keenye kufikia malengo, “amesema.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza, Mkuu wa Chuo cha Kodi Mamlaka ya mapato Tanzania (ITA),Prof.Isaya Jairo amesema Chuo chao kimetengeneza wataalamu wengi wa forodha ya kodi yenye misingi ya kujenga umahiri kwenye kukuza uchumi wa Taifa.
Amesema takribani wanafunzi 147 wameweza kuhitimu katika chuo hicho kupitia kozi mbalimbali ikiwemo Stashahada,Shahada na Stashahada ya Uzamilikwa wahitimu hao wa mwaka wa masomo 2023/2024.
Jairo amesema kati ya wahitimu hao 417 wahitimu 236 ni wa kiume na wahitimu 181 ni wa kike ambapo wahitimu 195 watatunukiwa cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki yaani the East African Customs and Freight Fowarding Practising Certificate (EACFFPC).
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Kodi Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema baraza lililopo liendelee kufanya kazi ili kufanikisha watumishi ambapo itawezesha kuongeza idadi ya walipa kodi pamoja na kuongeza ulipaji kodi kwa nchi na wataendelea kuboresha miundombinu ili watoe wahitimu bora kwa maendeleo ya nchi.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano