Na Esther Macha,TimesMajira,Online Iringa
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Iringa ,Dkt.Robert Salim amesema kwa kushirikiana na serikali na wadau wamewezesha upatikanaji wa chanjo zote za kuzuia magonjwa yanayozuilika ili kuweza kuepusha vifo .
Ametaja magonjwa yanayolengwa na mpango wa Taifa wa chanjo kuwa ni kifua kikuu ,Dondakoo,kifaduro ,polio,surua ,Rubella,Pepopunda,Homa ya ini,homa ya uti wa mgongo,kichomi,kuhara na saratani ya mlango wa kizazi .
Pia amesema wameweza kufika kiwango cha uchanjaji kwa asilimia 99,ambayo ni hatua kubwa iliyofikiwa kwa serikali ya awamu ya tano katika kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.
Akifungua semina ya siku moja kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi wa kinga Wizara ya afya ,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Robert Salimu amesema hayo hivi karibuni katika semina ya siku moja kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Mbeya,Iringa,Njombe,pamoja na Ruvuma.
Dkt.Salim amesema kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kushirikiana na shirika la Gavi,wadau na wadau wengine wa maendeleo imefanikiwa kununua magari 74.
Ametaja aina ya magari hayo kuwa ni Fork lift tatu ,generate moja vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh.Bilion 7 kwa ajili ya kuimarisha huduma za chanjo hapa nchini.
Amesema kuwa kati ya magari 74 yaliyonunuliwa magari 61 ni aina ya Toyota Pickup ambayo kila moja ina thamani ya sh.milioni 56.6 kwa ajili ya kuimarisha usambazaji wa chanjo katika halmashauri 61hapa nchini.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi