Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa filamu mwenye mvuto wa aina yake na mjasiriamali hapa nchini, Irene Uwoya amewataka Watanzania kupunguza roho mbaya kwani haitawasaidia kitu pindi pale mmoja wapo anamzidi mwengine kwa kila kitu.
Akitoa ujumbe huo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram, Uwoya amesema Watanzania wanatakiwa kukubali iwapo mtu atakuzidi kwa kila hali ili kuishi bila ya fikra potofu.
“Wabongo punguzeni roho mbaya haitawasaidia kitu, mtu akikuzidi kubali huyu kanizidi acha kutafuta kasoro hazina kichwa wala miguuu. Wengi wenu mnashindwa kufanikiwa sababu mpo busy kushusha wenzenu na kuwatafutia kasoro badala ya kujiombea mambo yako yaenda.
“Baraka zako zipo kwa watu wanavyokuombea sasa wewe toka uzaliwe huna zuri unawazia wenzako vibaya, una tafuta kasoro za watu huwezi fanikiwa maisha. Huo muda unatumia kuchukia watu embu muombe Mungu abadilishe maisha yako.
“Huwezi kupanda kwa kumshusha mwenzako, utabaki unalalamika tu Mungu nimekosea wap kumbe roho yako mbaya ndio inakuponza, jifunze kwa walio kuzidi acha chuki za kijinga hazitakusaidia unapoteza mda na baraka zako,” alisema Uwoya.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio