Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online.
HUKU maambukizi na vifo vikizidi kuongezeka kwa kasi nchini India baada ya wimbi la pili la ugonjwa COVID-19, baadhi ya raia nchini India wametoka na mbinu mpya ya kujisiliba kinyesi cha ng’ombe na mikojo ili kupambana na janga hilo.
Hata hivyo wataalamu wa afya wameendelea kutoa tahadhari kuwa hakuna ushahidi kuwa kufanya hiyvo inasaidia kupandisha kinga za mwili au hata kutibu COVID-19.
Shirika la Habari Reuters, lilimkariri Dr. JA Jayalal, ambaye ni Rais wa Taasisi ya Dawa nchini India (Indian Medical Association) akieleza kuwa “kuna uwezekano mkubwa wa kudhurika kiafya iwapo mtu atajisiliba na kujipaka kinyesi cha ng’ombe kwani magonjwa mengine yaweza kuhama kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu”
Kwa muujibu wa dini ya Hindu, ng’ombe ni ishara takatifu katika maisha na duniani. Ni jambo la kawaida kwa Wahindi kusujudu na kuabudu ng’ombe, na wengine hupita katika mazizi ili kuzoa na kujipaka kinyesi cha ng’ombe huku wakimkumbatia kwa heshma kwa mnyama huyo.
Baada ya kujipaka na kinyesi hicho muumini hujisafisha kwa kutumia maziwa au siagi.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria