Na Mwandishi Wetu
WASHINGTON, Shirika la Fedha Duniani (IMF) linatarajia kutoa dola bilioni 11 kwa nchi 32 za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zmeomba msaada kwa ajili ya kusaidia kupambana na virusi vya corona (COVID-19) na kuimarisha uchumi katika ukanda huo.
Hatua hizo za IMF na washirika wake ikiwemo Benki ya Dunia, Shirika la Afya Duniani (WHO), Benki ya Maendeleo ya Afrika na Umoja wa Afrika zinalenga kuunga mkono juhudi za ndani ikiwa ni pamoja na usaidizi kwa kaya zilizo hatarini,kuimarisha sera za kifedha na nyingine.
Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo barani Afrika, Abebe Aemro Selassie amebainisha hayo kupitia taarifa aliyoitoa ikiangazia mambo mbalimbali yanayohusiana na uchumi katika ukanda huo.
Kwa mujibu wa IMF, matatizo ya kiafya na kiuchumi ambayo hayajawahi kuonekana yanaweza kuzima ndoto za matarajio ya ukuaji wa kiuchumi katika ukanda huo kwa miaka ijayo, hivyo hatua za haraka zinahitajika.
Utabiri unaonyesha huenda uchumi katika ukanda huo ukaporomoka hadi kufikia asilimia 1.6 kwa mwaka 2020, matokeo ambayo yanatajwa kuwa mabaya zaidi katika rekodi za ukuaji uchumi.
Kwa habari hii kwa kina na nyingine nyingi jipatie nakala ya Majira.
More Stories
Dk. Mpango amwakilisha Samia sherehe za Uhuru wa Lesotho
Madaktari bingwa wa Samia watua Rukwa
Utashi wa Rais Samia na matokeo ya kujivunia vita dawa za kulevya nchini