December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Imani potofu kikwazo ugonjwa wa kutokwa na damu bila kuganda (HAEMOPHILIA)

Na Aveline Kitomary, TimesMajira Online, Dar es Salaam

JAMII imetakiwa kuacha kuwa na imani za kishirikina na badala yake  kujitokeza kupima ugonjwa wa kutokwa na damu muda mrefu bila kuganda(Haemophilia) kwani ugonjwa huo unatibika.

 Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam,  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Rashid Mfaume,  wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa  wataalam wa afya  juu ya haemophilia amesema kuendelea kuwepo kwa imani potofu  kwa wananchi nchini kunapelekea ongezeko la ugonjwa ndani ya jamii kwani wengi wamekuwa wakiamini kuwa Haemophilia utokana na watu kulogwa.                                                         

Amesema changamoto ya ukosefu wa elimu ya ugonjwa  huo bado ni kubwa nchini.

“kutokana  na changamoto hiyo  tumekuwa  tukiendelea kutoa elimu kwa wataalam wa afya na wananchi  kupitia vyombo vya habari ilikuweza  kutambua ugonjwa huo kwa haraka ilikuweza kupata matibabu kwa haraka,” amesema

Amesema ukosefu wa elimu kwa wananchi  kumekuwa kukisababisha watu wengi wanaopata ajali kutokwa na damu nyingi bila kupata ufumbuzi wakati kama wangejua tatizo mapema wangetibiwa.

“  Kwa mujibu wa ta kwimu tulizo nazo zinaonyesha watu wenye ugonjwa huo ni kati ya asilimia 80 hadi 85 hivyo kwa nchi yetu inaonyesha kati ya watu milioni 60 waliopo nchini watu 6000 hadi 12000 ndio wenye ugonjwa huo na waliogunduliwa na kupatiwa  matibabu ni 167 mpaka sasa nchi nzima,”amesema

 amesema kwa mujibu wa  takwimu za mkoa wa Dar es Salaam za sense ya mwaka 2012  zinaonyesha  kwa watu milioni 6 , watu 600 wanakadiliwa kuwa ugonjwa huo ambapo watu 60 tu ndio wanaendelea na matibabu.

“Ukosefu huo wa elimu umepeleka baadhi ya watanzania wengi  kukimbilia kwa waganga wa kienyeji pale wanapopata majeraha nakupelekea kutokwa na damu kwa muda mrefu bila kuacha,” alisema

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kutokwa na damu nchini Stella Rwezaula  ambaye pia  ni Mkuu wa kitengo cha magonjwa hayo, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH)  alibainisha kuwa  bado kuna changamoto ya wataalam wa afya wa ugonjwa huo nchini.

“ Wataalam  afya  wa mikoani bado hawafaham namna ya kutibu ugonjwa huo hivyo ndio maana wameanza kutoa elimu kuanzia kwa mkoa wa Dar es Salaam kisha baada ya hapo watazunguka kutoa elimu mikoani,” ameeleza.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Stella Rwezaura akizungumzia ugonjwa wa Haemophilia

Pia amesema wataendelea kufanya kazi kwa ukaribu na         Wizara   ya  Afya ilikuhakikisha kuwa magonjwa hayo ya kutokwa na damu yanawekwa kwenye mpango kazi wa miaka mitano ya magonjwa yasiyoambukiza  ilikuweza kuandaa mwongozo kwa wataalam wa afya wa mikoani.

Dk.Stella alisema kwa asilimia kubwa ugonjwa huo ni wakurithi japo kwa asilimia 30 huweza kusababishwa na mabadiliko yasiyo ya kawaida  ya vinasaba  na kusema  na ugonjwa huo hivyo ni vyema watu wakajitokeza kupima ugonjwa huo.

“Dalili za ugonjwa huo nipamoja na kutokwa na damu kwa muda mrefu bila kuganda kuanzia utotoni endapo  mtu kufanyiwa upasuaji au kupata jeraha.

 “Kwa watoto wachanga wanaozaliwa  na ugonjwa damu yao kuchelewa kuganda pale anapokatwa kitovu, anapo ng’oa jino, kutokwa na damu mikononi na  magotini wakati wa kutambaa  tofauti na wengine, kuvimba magoti na viwiko jambo ambalo upelekea ulemavu wa kudumu, , “ amefafanua .

Dk.Stella amesema wakati mwingine ugonjwa huo husababisha watu kupoteza maisha  kutokana na kuvuja damu tumboni na kichwani bila kujua kama ugonjwa huo hivyo nivyema kuwahi kituo cha afya.